Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City waambiwa Pep Guardiola apewe kazi mpya

MAN CITY Pict

Muktasari:

  • Guardiola ana mkataba na Man City hadi mwisho wa msimu wa 2026/27, lakini kumekuwa na taarifa za mara kwa mara zikidai anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA Stuart Pearce amewaambia mabosi wa Manchester City kuhakikisha wanafikiria kumbakiza Pep Guardiola klabuni kama mkurugenzi wa michezo pale atakapoamua kuachia ngazi ya ukocha mkuu.

Guardiola ana mkataba na Man City hadi mwisho wa msimu wa 2026/27, lakini kumekuwa na taarifa za mara kwa mara zikidai anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 amekuwa akiinoa Man City tangu mwaka 2016 na ameisimamia katika kipindi chenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, akitwaa mataji sita ya Ligi Kuu England, mawili ya Kombe la FA, manne ya Kombe la Ligi, Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Kombe la Dunia la Klabu.

Alisaini mkataba mpya Novemba 2024 unaomalizika Juni 2027, lakini uvumi umeongezeka miezi ya hivi karibuni. Man City tayari imeanza mchakato wa kutafuta mrithi, huku aliyekuwa msaidizi wake wa zamani, Enzo Maresca, akiingia kwenye mipango ya klabu hiyo baada ya kuondoka Chelsea, Januari mwaka huu.

Pearce, aliyeinoa Man City kati ya mwaka 2005 na 2007, anaamini klabu hiyo inapaswa kufanya kila iwezalo kumbakiza Guardiola kwa nafasi yoyote ile pale atakapoondoka katika jukumu lake la sasa.

Pearce amesema: “Ukitazama klabu zote za soka duniani na jinsi baadhi yao zilivyo imara, Manchester City ni miongoni mwa klabu zilizo imara zaidi. Kwa upande wa kocha, huoni wamiliki wakikimbilia kutafuta vichwa vya habari. Lakini, itakuwa kazi kubwa sana kumrithi atakapoondoka.

“Iwapo watatafuta mrithi wa aina yake moja kwa moja, wana klabu shirika duniani kote, lakini je, wana makocha katika klabu hizo wanaoweza kuja kuchukua nafasi kutoka klabu zao nyingine? Hilo linaweza kuwa jambo la kuzingatia siku zijazo. Mabadiliko makubwa ya mtindo wa uchezaji yanaweza kuwarudisha nyuma kidogo.”