Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City kuvunja rekodi kwa Wirtz

Muktasari:

  • Staa huyo wa Bayer Leverkusen, 22, aliwasili Blackpool akitokea Maastricht huko Uholanzi, wakati Man City ikipambana kuipiga kikumbo Bayern Munich kwenye vita ya kunasa saini yake.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola afanya mazungumzo na kiungo mchezeshaji Florian Wirtz wakati miamba hiyo ya Etihad ikitaka kuweka rekodi ya kumnasa Mjerumani huyo kwa Pauni 126 milioni.

Staa huyo wa Bayer Leverkusen, 22, aliwasili Blackpool akitokea Maastricht huko Uholanzi, wakati Man City ikipambana kuipiga kikumbo Bayern Munich kwenye vita ya kunasa saini yake.

Wirtz, akiwa mmoja wanasoka wanaosakwa sana Ulaya kwa sasa alisafiri na wakala wake ambaye ni baba yake kwenda kuweka sawa mipango ya kujiunga na wababe hao wa Etihad.

Kocha Guardiola anamtazama Wirtz kama chaguo lake namba moja kwenye wachezaji ambao Man City itajijenga kumzunguka wakati gwiji Kevin De Bruyne, 33, atakapoachana na timu hiyo mwisho wa msimu huu kutokana na mkataba wake kufika tamati Juni.

Ofa ya Man City kwenye mpango wa kunasa saini ya staa huyo inaweza kuweka rekodi ya uhamisho England, kuvunja ile ya Pauni 115 milioni, ambayo Chelsea ililipa huko Brighton kunasa huduma ya kiungo wa kati, Moises Caicedo mwaka 2023.

Wirtz, baba na mama yake Karin walisafiri kwa ndege binafsi kutoka uwanja wa ndege wa Maastricht-Aachen huko Uholanzi kwenda Blackpool, kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild. Baada ya hapo walitumia usafiri wa gari hadi Manchester kukutana na Guardiola kabla ya kurudi.

Waliamua kutumia uwanja huo mdogo wa ndege uliopo kwenye mpaka wa Ujerumani na Uholanzi ili kuzuia jambo hilo lisifahamike na wengi, lakini gazeti la Bild lilifanikiwa kupata picha za mama na baba yake Wirtz kwenye uwanja wa ndege wa Uholanzi wakati alipokuwa wakirudi. Leverkusen ipo tayari kumuuza Wirtz kwenda Man City kuliko kuwauzia silaha wapinzani wao, Bayern.