Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City kukamuliwa ndefu kwa Marmoush

Tetesi Pict

Muktasari:

  • Man City ambayo awali ilidaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 50 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba wake sasa huenda ikatumia kiasi kikubwa zaidi ya hicho.

MANCHESTER City huenda ikalazimika kutoa kiasi kikubwa cha pesa ili kufanikisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na Misri, Omar Marmoush, 25, kwa sababu timu yake haitaki kumwachia kwa sasa kwani inapambana kwa ajili ya kumaliza ndani ya nafasi nne za juu na kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Man City ambayo awali ilidaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 50 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba wake sasa huenda ikatumia kiasi kikubwa zaidi ya hicho.

Mkataba wa sasa wa Omar unaisha 2027 na amekuwa akihusishwa na timu nyingi kwa sababu ya kiwango kikubwa alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amecheza mechi 24 za michuano yote na kufunga mabao 18. Kati ya mambo ambayo yameivutia sana Man City kiasi cha kutaka kumsajili ni uwezo wake wa kufunga na kusaidia wenzake kufunga.


Amad Diallo

WINGA wa Manchester United, Amad Diallo, 22, amefikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika timu hiyo na anatarajiwa kukamilisha mchakato huo wiki ijayo.

Diallo ambaye ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Man United kwa sasa, anadaiwa kuwa atakunja zaidi ya Pauni 100,000 kama mshahara kwa wiki kupitia mkataba huo mpya.


Nuno Mendes

MANCHESTER United inataka kuuza baadhi ya wachezaji wake kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kumsajili beki wa Paris St-Germain na Ureno, Nuno Mendes, 22, katika dirisha hili.

Nuno ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha PSG msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


Bryan Mbeumo

STRAIKA wa Brentford na Cameroon, Bryan Mbeumo, 25, yupo katika orodha ya mastaa ambao Arsenal inataka kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji.

Mbeumo anahusishwa na timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango chake msimu huu. Mkataba wake unaisha mwisho wa msimu. Amecheza mechi 23 na kufunga mabao 13.


James McAtee

BAYER Leverkusen, RB Leipzig, Mainz, Borussia Dortmund na Stuttgart zote zinapambana kuhakikisha zinaipata huduma ya kiungo wa Manchester City, James McAtee, 22, katika dirisha hili. Man City inadaiwa kuwa tayari kumwachia fundi huyu kwa mkopo ama jumla lakini kwa timu itakayokuwa tayari kufikia makubaliano yao ikiwa kwa mkopo kulipa mshahara wake wote.


Marcus Rashford

KWA mujibu wa tovuti ya Sky Sports, Manchester United inafahamu kwamba wawakilishi wa mshambuliaji wao raia wa England, Marcus Rashford, kuwa wapo katika mazungumzo na mabosi wa AC Milan kwa ajili ya dili la mchezaji huyo kutua kwenye timu hiyo kwa dirisha hili. Rashford mwenye umri wa miaka 27, kwa sasa amewekwa nje ya kikosi.


Oleksandr Zinchenko

INTER Milan inajiandaa kuwasilisha ofa kwenda Arsenal ili kumsajili beki wa timu hiyo na Ukraine, Oleksandr Zinchenko, 28, katika dirisha hili.

Zincheko amepewa ruhusa ya kuondoka Januari hii ama mwisho wa msimu ikiwa tu atapata timu itakayokuwa tayari kumsajili na kulipa ada yake ya uhamisho inayokadiriwa kufikia Euro 30 milioni.


Antony

WINGA wa Manchester United na Brazil, Antony, 24, amekataa ofa ya kujiunga na Olympiakos ya Ugiriki ambayo ilihitaji kumsajili katika dirisha hili.

Antony ambaye hapati nafasi katika kikosi cha Man United, licha ya kukataa ofa hiyo bado anahitaji kuondoka Manchester lakini lengo lake ni kujiunga na timu zilizopo kwenye ligi tano bora barani Ulaya.