Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamelodi Sundowns mabingwa wapya CAFCL

Muktasari:

  • Mamelodi Sundowns imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili ambapo mara ya kwanza ni 2016 na mara ya pili ni msimu huu.

Mamelodi Sundowns imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na FAR Rabat nchini Morocco jana, Jumapili, Mei 24, 2026.

Sare hiyo katika mechi hiyo ya marudiano ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdallah jijini Rabat, Morocco, imeifanya Sundowns kutwaa ubingwa kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.

Sundowns imebebwa na ushindi wa bao 1-0 ilioupata katika mechi ya kwanza nyumbani Afrika Kusini wiki iliyopita.

Katika fainali iliyomalizika muda mfupi uliopita, FAR Rabat ndio wametangulia kupata bao la uongozi kupitia kwa Mohammed Hrimat katika dakika ya 40.

Hata hivyo kabla ya filimbi ya mapumziko, Teboho Mokoena aliisawazishia Mamelodi Sundowns na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare.

Katika kipindi cha pili, FAR Rabat walionekana kulishambulia kama nyuki lango la Mamelodi Sundowns lakini hawakuweza kupata bao.

FAR Rabat ingeweza kupata bao la pili kupitia mkwaju wa penalti ambao walipata lakini Hrimat alipiga shuti lililookolewa na kipa Ronwen Williams.

Licha ya Refa Omar Artan kutoka Somalia kuongeza dakika nane, matokeo ya mchezo huo hayakubadilika.

Kwa kutwaa ubingwa huo, Mamelodi Sundowns inakuwa imechukua taji hilo kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni 2016.