Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo yameanza kuchangamka, Cunha atua Manchester

Muktasari:

  • Katika picha zilizopigwa, Cunha alikuwa amevaa fulana nyeupe na kofia ya baseball ya Los Angeles. Alikuwa ameongozana na mkewe mjamzito, Gabriela, na mtoto wao wa kiume.

Manchester England. Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Matheus Cunha, mwenye umri wa miaka 26, ameonekana akiondoka katika hoteli ya kifahari ya The Lowry jijini Manchester.

Hoteli hiyo ipo karibu kabisa na kituo cha mazoezi cha United, Carrington jambo linaloashiria kuwa mchakato wa usajili umefikia ukingoni.

Katika picha zilizopigwa, Cunha alikuwa amevaa fulana nyeupe na kofia ya baseball ya Los Angeles. Alikuwa ameongozana na mkewe mjamzito, Gabriela, na mtoto wao wa kiume. Gabriela alimuongoza mtoto wao hadi kwenye gari lililokuwa linawasubiri nje ya hoteli.

Cunha, ambaye alifunga mabao 15 katika mechi 33 za Ligi Kuu ya England msimu uliopita akiwa na Wolverhampton, amekuwa katika kiwango bora ambacho kilimfanya Ruben Amorim kuwashawishi mabosi wa United wamvute Old Trafford mshambuliaji huyo.

Manchester United inatarajia usajili huu utamletea kocha mpya Rúben Amorim nguvu mpya safu ya ushambuliaji, hasa baada ya ziara yao ya mwishoni mwa msimu nchini Malaysia kugubikwa na sintofahamu na matukio tata.

Hii ni hatua ya kwanza ya mipango ya Amorim kufufua kikosi baada ya United kumaliza msimu kwa nafasi mbaya zaidi katika historia ya Ligi Kuu.

Cunha anatarajiwa kuwa chaguo la kwanza katika safu ya ushambuliaji, huku mazungumzo yakiendelea juu ya mustakabali wa baadhi ya nyota waliopo sasa, akiwemo Marcus Rashford.

Cunha na mkewe Gabriela, walifunga ndoa 2023 nchini Brazil. Cunha sasa anasubiri kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kutangazwa rasmi.