Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo ya kifamilia kumuondoa Walker City

Walker Pict

Muktasari:

  • Katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kukosekana katika mchezo wa FA dhidi ya Salford City ambao ulimalizika kwa timu yake kushinda mabao 8-0, Pep Guardiola alifichua kwamba alimweka nje staa huyo kwa sababu alimwambia kwamba anafikiria kuondoka.

MANCHESTER, ENGLAND: INAELEZWA beki wa Manchester City, Kyle Walker aomba kuondoka katika timu hiyo katika dirisha hili kutokana na sababu za kifamilia akitaka kuwa sehemu ambayo anaweza kutulia na kujaribu kujenga upya familia yake baada ya sintofahamu zilizotokea mwaka jana.

Katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kukosekana katika mchezo wa FA dhidi ya Salford City ambao ulimalizika kwa timu yake kushinda mabao 8-0, Pep Guardiola alifichua kwamba alimweka nje staa huyo kwa sababu alimwambia kwamba anafikiria kuondoka.

“Siku mbili zilizopita Kyle aliomba kuangalia uwezekano wa kuondoka na kujiunga na timu ya nje ya nchi, aliwahi kuomba hili miaka miwili iliyopita baada ya ushindi wa makombe matatu. Bayern Munich walimtaka lakini ofa yao haikuwa ya kutosha. Hatuwezi kutaja mafanikio ambayo timu imeyapata bila ya kutaja jina lake, ametupa mchango mkubwa sana,”alisema Guardiola.

“Lakini sasa katika mawazo yake amesema angependa kutazama uwezekano wa  kwenda nchi nyingine. Kwa sababu hiyo, napendelea kuwachezesha wachezaji wengine ambao akili zao ziko hapa,”

Ripoti kutoa Daily Mail zinaeleza kwamba, kuna baadhi ya timu za Saudi Arabia zimeonyesha nia ya kumsajili staa huyu mwenye umri wa miaka 34 na kumpa mshahara wa zaidi ya Pauni 400,000 kwa wiki.

“Alienda kwenye ofisi za timu kuomba hili ingawa hajasema kama ana ofa au anaondoka, ila ameomba kuangalia uwezekano na kufikiria, hivyo hatuwezi kujua huenda asiondoke, lakini vyovyote itakavyokuwa mimi naheshimu mawazo yake. Ninashukuru sana kwa kile alichofanya kwa miaka mingi kwetu. Alikuja miaka minane iliyopita nasi tukaanza kushinda, kushinda, kushinda na amekuwa muhimu kwa timu ya taifa pia.”

Mail Online iliripoti Ijumaa kwamba mke wa Walker, Annie Kilner, ameachana na mpango wa kutaka kutalikiana na staa huyo, pia amemruhusu kurudi kwenye nyumba yao.

Walker na Annie waliingia katika sintofahamu Agosti mwaka jana baada ya dada huyo kugundua kwamba mumewe amezaa nje ya ndoa na mrembo Lauryn Goodman.


Baada ya kugundua hilo, Annie aliwasilisha maombi ya talaka, pia Walker ikatakiwa atoke kwenye nyumba waliyokuwa wanaishi.

Vyanzo vinasema Annie, ameamua kumsamehe Walker na sasa anafanya kila linalowezekana kuhakikisha penzi linarudi kama zamani.

Hii ndio inaelezwa kuwa sababu ya Walker kutaka kuondoka England kwenda mahali ambako yeye na mkewe watakuwa wapya mbele ya macho ya watu na kwenye utulivu zaidi kwa ajili ya kuhakikisha wanarudi kama ilivyokuwa zamani.