Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matamu baada ya Arsenal kushusha kipigo kizito kwa Man City

Matamu Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha Kocha Mikel Arteta sasa kimebakiza pointi sita tu kuishika Liverpool kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England baada ya ushindi wao wa kibabe kabisa dhidi ya Man City uwanjani Emirates, juzi Jumapili.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imeonyesha bado imo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Manchester City mabao  5-1 katika mechi ambayo Kocha Pep Guardiola na kikosi chake aliteseka mwanzo mwisho.

Kikosi hicho cha Kocha Mikel Arteta sasa kimebakiza pointi sita tu kuishika Liverpool kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England baada ya ushindi wao wa kibabe kabisa dhidi ya Man City uwanjani Emirates, juzi Jumapili.

Bila shaka, ushindi huo wa Arsenal utakuwa unaongeza presha kubwa kwa Kocha Arne Slot na kikosi chake cha Liverpool, ambacho kama kitashindwa kutumia vyema kiporo chao dhidi ya mahasimu wao wa Merseyside, Everton wiki ijayo, basi vita ya ubingwa utakuwa tamu zaidi.

Everton kwa sasa ipo chini ya kocha mwenye uzoefu, David Moyes, jambo linalofanya kuwapo na matarajio ya kuwa Liverpool itakuwa na shughuli pevu.

Man City, kwa upande wao, kipigo hicho kimewafanya waachwe pointi 15 na vinara Liverpool na pointi tisa nyuma ya Arsenal.

Kwa sasa hakuna anayeifikiria Man City itakuwa hai kwenye mbio za ubingwa na sasa inapambana vita ya kuwania kuwapo kwenye Top Four ili kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

“Ilikuwa mechi kubwa na tulikuwa kwenye kiwango cha juu,” alisema nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard baada ya kuwachapa Man City.

“Kwa kelele zile za mashabiki na ufungaji ule wa mabao hakuna kitu kizuri kinachozidi kile jambo.”

Odegaard ndiye aliyefunga bao la kuongoza kwenye sekunde ya 103 tu baada ya beki Manuel Akanji kufanya kosa.

Kutokana na kile kilichotokea kwenye mchezo huo wa Arsenal na Man City, hizi hapa takwimu matata kabisa zilizotokana na kipute hicho cha Emirates.


  • Ukimweka kando Havertz aliyekosa nafasi ya wazi ya kufunga kwenye kipindi cha kwanza, Arsenal haikuwa makini sana kwenye kupasia mipira nyavuni. Imefunga mabao matano kwenye mechi hiyo ambayo ingefunga mara nyingi zaidi kutokana na kutengeza nafasi nyingi kuwazidi Man City.


  • Safu ya kiungo na ushambuliaji iliyoanzishwa na Arsenal kwenye mechi hiyo, Leandro Trossard peke yake ndiye hakuhusika kwenye kuasisti au kufunga katika kipute hicho. Declan Rice aliasisti mara mbili, Thomas Partey alifunga, Martin Odegaard alifunga, Gabriel Martinelli aliasisti na Kai Havertz alifunga na kuasisti.


  • Mabao yote matano yaliyofungwa na Arsenal yalifungwa kwa Man City kutafutwa uwanjani, hakuna bao hata moja la mpira wa kutenga.


  • Ethan Nwaneri (miaka 17, miezi 10, siku 12) ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao dhidi ya bingwa mtetezi kwenye Ligi Kuu England… Myles Lewis-Skelly alifunga bao la tatu la Arsenal. Lakini, Lewis Skelly ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo tangu Wayne Rooney alipoifungia Everton dhidi ya Arsenal ya Arsene Wenger, Machi 2003 (miaka 17, miezi 5)


  • Erling Haaland amegusa mpira mara tisa tu kwenye mechi yote. Lakini, Nwaneri aligusa mpira mara 11 baada ya kuingia dakika 84.


  • Declan Rice amepiga pasi muhimu nne (pasi za mwisho kabla ya wachezaji wenzake kupiga mashuti golini). Hiyo ilikuwa pasi moja tu pungufu ya pasi muhimu zilizopigwa na kikosi kizima cha Man City.


  • Manchester City sasa imeruhusu mabao manne au zaidi mara nne tofauti ndani ya msimu huu. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Man City ya Pep Guardiola kwa muda wote aliyokuwa na kikosi hicho cha Etihad kuruhusu kichapo cha mabao matano.


  • Hicho ni kipigo kizito kwa Man City kwa mechi za ugenini kwenye Ligi Kuu England kwa kipindi cha zaidi ya miaka minane – ikianzia kwenye kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Everton na ulikuwa msimu wake wa kwanza Guardiola (Januari 2017).


  • Arsenal sasa imeweka rekodi yake tamu ya kucheza mechi nyingi za Ligi Kuu England bila kupoteza chini ya kocha Mikel Arteta. Arsenal haijapoteza katika mechi 14 za mwisho, mara ya mwisho kwenda mechi nyingi bila ya kupoteza, ilikuwa kuanzia Agosti hadi Desemba 2018 chini ya kocha Unai Emery.


  • Arsenal imepata ushindi wa mechi mbili mfululizo ilipocheza nyumbani dhidi ya Manchester City kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2008-09 – wakati huko nyuma iliwahi kushinda mechi nne mfululizo kabla ya Man City haijachukuliwa na tajiri wa Kiarabu msimu wa 2005-06.


  • Man City ya Pep Guardiola iliichapa Arsenal kwenye mechi 12 mfululizo kwenye ligi kati ya 2017 na 2023. Kwa sasa imeshindwa kuwafunga kwenye mechi ya nyumbani na ugenini kwa misimu yote miwili ya mwisho.


  • Kichapo kwa Arsenal cha mabao 4-1 ilichokipata kutoka kwa Man City, siku 649 zilizopita, kwa mana maana ya Aprili 2023 kilikuwa cha mwisho wa timu hiyo kuchapwa kwa mabao mengi na wababe wenzao wa Big Six kwenye Ligi Kuu England. Kwa sasa haijapoteza kwa karibu miaka miwili kwenye mechi za Big Six, ikiwa imecheza mechi 18. Hakuna timu iliyovuna pointi nyingi kwenye mechi za Big Six msimu huu kuwazidi Arsenal, hata Liverpool hawaoni ndani.


  • Mabao 5-1 ni ushindi mkubwa zaidi kupata Arsenal kwenye ligi msimu huu wa 2024-25 na utamu zaidi imefanya hivyo dhidi ya mabingwa watetezi. Kwa kifupi ni ushindi mkubwa zaidi kwa Arsenal kupata dhidi ya timu inayoshikilia ubingwa wa Ligi Kuu England.