Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamadou Gaye awatuliza mashabiki Nigeria, aitaka FIFA kuamua

ONANA Pict

Muktasari:

  • Nigeria ambayo inafahamika pia kwa jina la Super Eagles ilipoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penalti, lakini baadaye ililalamika FIFA, ikidai wachezaji wa DR Congo, Axel Tuanzebe na Aaron Wan-Bissaka hawakustahili kucheza mechi hiyo kwa kukosa vigezo vya uraia.

MTAALAMU wa soka barani Afrika, Mamadou Gaye, amewaomba wadau wa soka kuendelea kuwa wavumilivu wakati Nigeria ikisubiri uamuzi kutoka FIFA katika kesi dhidi ya DR Congo inayodaiwa kukiuka utaratibu wa kuwatumia baadhi ya wachezaji waliokosa sifa, wakati wa mechi ya mchujo wa Kombe la Dunia 2026, iliyochezwa mwishoni mwa mwaka jana nchini Morocco.

Nigeria ambayo inafahamika pia kwa jina la Super Eagles ilipoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penalti, lakini baadaye ililalamika FIFA, ikidai wachezaji wa DR Congo, Axel Tuanzebe na Aaron Wan-Bissaka hawakustahili kucheza mechi hiyo kwa kukosa vigezo vya uraia.

Hadi sasa, FIFA bado haijatangaza uamuzi wowote, jambo ambalo limeacha mashabiki, wachezaji, na Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) katika hali ya sintofahamu ya sakata hilo ambalo linaonekana huenda likawa mkombozi kwa Nigeria.

Gaye ameeleza kuwa timu ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana, ilipoteza pointi tatu katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya FIFA kugundua ilitumia mchezaji asiye halali, Teboho Mokoena, na uamuzi huo ulitolewa kabla ya mechi za mwisho za Kundi C.

“Tuisubiri FIFA kutoa uamuzi wake. Kumbukeni pointi ilizopokwa Bafana Bafana dakika za mwisho,” amesema Gaye kwenye kipindi cha SuperSport Soccer Africa. 

Gaye ameongeza kuwa, kesi ya Nigeria inapaswa kuendelea kama ilivyopangwa, na kuongeza kuwa timu yoyote itakayopoteza kesi hiyo bado FIFA inaweza kukatiwa rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Iwapo FIFA itatoa uamuzi wa mwisho, DR Congo itacheza na mshindi wa mechi ya mchujo kati ya New Caledonia na Jamaica, na mshindi wa mechi hiyo atapata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia.