Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

John Mikel Obi: Mourinho amenishangaza, hakutakiwa kuzungumza vile

OBI Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo lilitokea katika mechi ya mchujo ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa wiki iliyopita mjini Lisbon, ambapo Vinicius Jr alidai kubaguliwa na mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni, akidaiwa kumwita “kima” (monkey). 

ALIYEKUWA nahodha na kiungo wa timu ya taifa ya Nigeria, John Mikel Obi, amelaani kauli ya kocha wa Benfica, Jose Mourinho, kuhusu sakata la ubaguzi wa rangi linalomuhusisha kiungo mshambuliaji wa Brazil na Real Madrid ya Hispania, Vinicius Jr.

Tukio hilo lilitokea katika mechi ya mchujo ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa wiki iliyopita mjini Lisbon, ambapo Vinicius Jr alidai kubaguliwa na mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni, akidaiwa kumwita “kima” (monkey). 

Baada ya mchezo, Mourinho alisema kwamba mchezaji huyo alihamasisha mashabiki wa Benfica alipokuwa akishangilia baada ya kuifungia bao la kuongoza Real Madrid. 

Kocha huyo raia wa Ureno alitoa mfano wa urithi wa Benfica kupitia hadithi ya mchezaji wa zamani, Eusébio, kama ushahidi kwamba klabu hiyo haina ubaguzi wa rangi.

Mikel Obi, ambaye aliwahi kucheza chini ya Mourinho katika nyakati tofauti akiwa Chelsea, ameeleza kwenye kipindi chake cha Obi One Podcast: “Nilitarajia kusikia maneno mazuri kutoka kwa kocha wangu wa zamani, lakini imenishangaza. Ndiyo, hili linafanyiwa uchunguzi, lakini hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi hapa, hakuna nafasi ya jambo kama hili, tusubiri hadi uchunguzi ukamilike.

“Hivyo, yeye kusema Vinicius Jr hakutakiwa kushangilia mbele ya mashabiki wa Benfica sio sawa, alipaswa kutafuta jambo linguine la kuzungumza mbele ya waandishi wa habari."

Kauli ya Mikel Obi inaonyesha kukinzana kwa mtazamo wa Mourinho kuhusu ubaguzi wa rangi, huku ikisisitiza umuhimu wa viongozi wa soka kueleza msimamo dhidi ya ubaguzi wa rangi kwenye michezo ya kimataifa na vilabu.

Wakati huohuo, mchezaji chipukizi Gianluca Prestianni hatakuwa sehemu ya kikosi cha Benfica kitakachoikabili Real Madrid katika mechi ya mkondo wa pili hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa kesho Jumatano, Februari 25, 2026.

‎Kinda huyo wa Argentina, anatuhumiwa kwa kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Vini Jr, wakati wa mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa mjini Lisbon, Ureno wiki iliyopita.