Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeraha yamstaafisha Mjapan wa Liverpool

Muktasari:

  • Nyota huyo anakabiliwa na jeraha la mguu lililoanza kijitokeza katika mechi ya Ligi Kuu ya England kati ya Liverpool dhidi ya Sunderland Februari 11, 2026, ikiwa ni ya mwisho kwa kiungo huyo kucheza kwa msimu huu.

KIUNGO wa Liverpool na timu ya taifa ya Japan, Wataru Endo ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa, ikiwa ni muda mfupi tangu aondolewe kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki Kombe la Dunia 2026, kutokana na kuandamwa na majeraha.

Nyota huyo anakabiliwa na jeraha la mguu lililoanza kijitokeza katika mechi ya Ligi Kuu ya England kati ya Liverpool dhidi ya Sunderland Februari 11, 2026, ikiwa ni ya mwisho kwa kiungo huyo kucheza kwa msimu huu.

Licha ya kucheza kwa dakika 45 katika ushindi wa Japan wa bao 1-0, dhidi ya Iceland kwenye mechi ya kirafiki, ila imeshindikana kwa nyota huyo kucheza Kombe la Dunia, ambapo kwa sasa ameamua rasmi kutundika daluga, huku nafasi yake ikichukuliwa na Shuto Machino.

Katika mtandao wa X zamani Twitter, nyota huyo alielezea masikitiko yake ya kukosa nafasi ya kucheza Kombe la Dunia, licha ya kuahidi ataendelea kuwa shabiki mkubwa wa kikosi hicho.

“Nimeondoka katika kikosi cha Kombe la Dunia, nikiwa nimehuzunika sana, nimefanya kila nilichoweza lakini zaidi ya hilo najivunia kuongoza timu hii kama nahodha tangu Kombe la Dunia la Qatar," amesema.

Nyota huyo alihitimisha kwa kusema ataendelea kuwa shabiki na kuiunga mkono timu ya taifa ya Japan katika michuano mbalimbali itakayoshiriki, hasa fainali za Kombe la Dunia 2026.

Japan inatarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza ya mashindano ya Kombe la Dunia 2026, dhidi ya Uholanzi siku ya Jumapili.

Timu hiyo ipo katika kundi moja la F na Sweden na Tunisia huku ikilenga kufuzu hatua ya mtoano, baada ya kuishia 16 Bora katika michuano miwili iliyopita ya Kombe la Dunia, huku ikiwa na kibarua cha kufika robo fainali mwaka huu kwa mara ya kwanza.