Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mexico yaanza kwa ushindi Kombe la Dunia, kadi nyekundu zikitawala

Muktasari:

  • Katika mchezo huo, imeshuhudiwa kadi nyekundu tatu zikionyeshwa ambapo mbili zimeenda upande wa Afrika Kusini na moja ikienda Mexico.

Timu ya Taifa ya Mexico imeanza vizuri kampeni za Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini.

Katika mchezo huo wa ufunguzi uliochezwa kwenye dimba la Azteca, Mexico City wenyeji Mexico walianza kuandika bao la uongozi mapema dakika ya tisa wakitumia vema makosa yaliyofanywa na beki Yaya Sithole.

Mshambuliaji Julián Quiñones ndiye ameandika rekodi ya kufunga bao la kwanza katika fainal za mwaka huu baada ya kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Afrika Kusini, Ronwen Williams.

Quiñones anaingia kwenye rekodi ya kufunga bao la kwanza katika mechi ya ufunguzi akiungana na mshambuliaji wa Ecuador, Enner Valencia ambaye alifanya hivyo katika fainali za 2022 zilizofanyika Qatar.

Katika mchezo huo, pia imeshuhudiwa kiungo wa Afrika Kusini, Teboho Mokoena akionyeshwa kadi ya kwanza ya njano baada ya kumchezea vibaya kiungo wa Mexico, Alvaro Fidalgo katika dakika ya 17 kabla ya kiungo mkabaji wa Mexico, Brian Gutierrez kuonyeshwa kadi ya pili ya njano katika mashindano hayo.

Mexico ilionekana kuwa bora zaidi ikifanya mashambulizi mengi kuelekea katika lango la Afrika Kusini ambao muda mwingi walionekana kuzuia mashambulizi ya wenyeji hao huku golikipa Williams akiokoa michomo hatari iliyokuwa ikipigwa na wapinzani wao.

Katika kipindi cha pili Mexico waliendelea na mashambulizi kwenye lango la Africa Kusini ambapo dakika ya 49 walifanya shambulio la hatari wakati kiungo Gutierrez alipopenyezewa pasi iliyowapita mabeki wa Afrika Kusini lakini hakuweza kufika langoni baada ya kufanyiwa madhambi na Sithole.

Sithole ambaye ndiye aliisababishia timu yake kufungwa bao la kwanza, alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo Wilton Sampaio kutoka Brazil. Kwa kuonyeshwa kadi hiyo beki huyo ameingiakwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu katika katika fainali za mwaka huu.

Mexico iliendelea kutafuta bao la pili ambapo kufikia dakika ya 67 mshambuliaji Raul Jimenez aliandika bao la hilo akimalizia pasi ya Roberto Alvarado. Bao hilo linakuwa la kwanza kwa mshambuliaji huyo katika mashindano ya Kombe la Dunia manne ambayo amecheza hadi sasa.

Themba Zwane naye alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 84 baada ya kumsukuma mchezaji wa Mexico wakati alipokuwa akikimbia bila mpira kuelekea kwenye lango la la wenyeji hao.

Haikuchukua muda baada ya refa kuonyesha tena kadi nyekundu wakati safari hii ikielekea upande wa Mexico ambapo beki César Montes alitolewa nje ya mchezo baada ya kumchezea vibaya beki wa kulia Afrika Kusini, Khuliso Mudau.

Hata hivyo, baada ya dakika 90 kumalizika Mexico iliondoka na ushindi huo ambao umeiweka kileleni mwa kundi A lenye timu nyingine za Korea Kusini na Jamhuri ya Zchek ambazo mchezo wao utaanza baadaye saa 11:00 alfajiri.