Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majanga! Uzi mpya Barca msimu ujao wavuja

BARCA Pict

Muktasari:

  • Wikiendi ijayo, blaugranas wataikabili Atletico Madrid saa 9:00 mchana katika mechi muhimu ambayo inaweza kuwa na athari kubwa katika kinyang’anyiro cha ubingwa kadri msimu unavyokaribia hatua ya mwisho.

BARCELONA, HISPANIA: JEZI mpya zinazotarajiwa kuvaliwa na Barcelona msimu ujao zinadaiwa kuvunja mapema na kuibua hofu kuwa huenda tayari zimeshayafikia magenge ya kimafia yanayoweza kuanza kuzitengeneza na kuzisambaza kabla klabu haijazizidua rasmi.

Hilo ni jambo linalojirudia miongoni mwa klabu kubwa za soka duniani, kwani kabla ya msimu wa sasa kumalizika, jezi za msimu ujayo mara nyingi huibuka hadharani kupitia uvujaji wa habari.

Kwa upande wa klabu hiyo ya Catalonia, kile kinachoonekana kuwa jezi mpya ya msimu wa 2026-27 kimeonekana, ingawa siyo rasmi. Kuna miundo mitatu mipya na yote inaonyesha utambulisho wa jadi wa klabu hiyo kubwa Hispania.

Jezi ya kwanza inafanana na ile ya sasa; hata hivyo, ina mstari wa wima ambao unatoa muonekano wa kisasa zaidi. Mara tu muundo ulipoibuka ulisababisha mwitikio mkubwa kutoka kwa mashabiki wa Jiji la Barcelona na duniani kote.

Chaguo la pili lililoandaliwa kwa msimu ujao linafanana kidogo na jezi ya Los Angeles Lakers, likijumuisha rangi maarufu ya zambarau ya timu hiyo ndani ya muundo wake, huku jezi ya tatu inawakilisha kurudi nyuma katika historia kwa mpangilio wa rangi ya bluu, jambo ambalo halijaonekana katika miaka miwili iliyopita.

Kwa sasa, kabla ya mapumziko, Barcelona inaongoza LaLiga ikifuatiwa kwa karibu na maadui wao wa kihistoria kwani

ina pointi 73, Real Madrid (69), Villarreal (58), Atletico Madrid (57) na Real Betis (44).

Wikiendi ijayo, blaugranas wataikabili Atletico Madrid saa 9:00 mchana katika mechi muhimu ambayo inaweza kuwa na athari kubwa katika kinyang’anyiro cha ubingwa kadri msimu unavyokaribia hatua ya mwisho.