Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona yapanga kukaa mezani na Lewandowski

Muktasari:

  • Mkataba wake wa sasa unamalizika katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, na Barcelona inaonekana kutaka kumbakisha kwa muda mfupi zaidi.

BARCELONA imepanga kumpa mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski, 37, mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao utahusisha kumpunguza mshahara lakini kutakuwa na bonasi kubwa kulingana na kiwango.

Mkataba wake wa sasa unamalizika katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, na Barcelona inaonekana kutaka kumbakisha kwa muda mfupi zaidi.

Hadi sasa Lewandowski bado hajafanya uamuzi wowote ikiwa atabaki Nou Camp au la, lakini inaelezwa kwamba ataamua hilo baada ya msimu kumalizika.

Barca inatamani huduma ya Lewandowski licha ya umri kumtupa mkono. Awali ilidaiwa kuwa huenda angeachwa ili kuweka nafasi ya kumsajili Rashford, lakini sasa mpango huo umesitishwa. Mabosi wa Barcelona wanaona imekuwa ngumu kuishawishi Man United ipunguze bei ya Rashford ya Pauni 26 milioni.


Bernardo Silva

KIUNGO wa kimataifa wa Ureno, Bernardo Silva, 31, anadaiwa kuwa na asilimia kubwa ya kuondoka Manchester City katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo mkataba wake utakuwa unamalizika. Hatua hiyo inaashiria mwisho wa kipindi chake ndani ya klabu hiyo ambayo imekuwa na mafanikio makubwa, huku Silva akiwa mmoja wa wachezaji muhimu. Haijafahamika wapi atatua baada ya kuondoka City na uamuzi wake unasubiriwa kwa hamu.


Carlos Baleba

KIUNGO wa kimataifa wa Cameroon, Carlos Baleba amechomoza tena katika orodha ya wachezaji ambao wanapigiwa upatu wa kuondoka katika kikosi cha Brighton mwishoni mwa msimu, lakini Manchester United iliyokuwa ikipambana kuinasa saini yake huenda ikakumbana na vita kutoka kwa Bayern Munich, Real Madrid, Barcelona na PSG ambazo tayari zimeonyesha nia ya kujitosa kuwania saini yake. Baleba amekuwa akitakiwa kwa udi na uvumba Man United.


Maxence Lacroix

BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Maxence Lacroix, 25, anafuatiliwa kwa karibu na klabu kadhaa kubwa zikiwemo Aston Villa, Bayern Munich, Chelsea na Liverpool. Lacroix kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Crystal Palace na kiwango chake cha ukabaji kimezivutia klabu nyingi ambazo zinataka kumsajili. Taarifa zinaeleza, Palace ipo tayari kumuuza fundi huyu lakini itahitaji zaidi ya Pauni 60 milioni ili kufanya hivyo.


Luis Suarez

LIVERPOOL na Newcastle United zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Luis Suarez, 28, anayekipiga katika klabu ya Sporting Lisbon. Suarez ameendelea kuvutia klabu kubwa kutokana na kiwango bora anachoonyesha Lisbon tangu msimu uliopita, na ameonyesha kuvutiwa zaidi na mpango wa kutua Ligi Kuu England kwani ni ndoto yake ya muda mrefu. Dili lake linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Casemiro

INTER Miami imeanza mazungumzo na wakala wa kiungo wa Brazil, Casemiro, 34, kuhusu kumsajili staa huyo aliyetangaza kuondoka Manchester United katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hata hivyo, Inter Miami inakabiliwa na ushindani kutoka klabu kadhaa za Ulaya pamoja na Saudi Arabia, jambo linaloweza kufanya dili lake kuwa gumu. Mazungumzo bado yako katika hatua za awali, na hatma ya Casemiro itategemea ofa atakazopokea.


Randal Kolo Muani

JUVENTUS inaangalia uwezekano wa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji kwa kumsajili straika wa PS-G na Ufaransa, Randal Kolo Muani, 27, dirisha lijalo la kiangazi. Kolo Muani kwa sasa yupo kwa mkopo katika kikosi cha Spurs lakini kiwango chake hakionekani kuivutia timu hiyo kumsainisha mkataba wa moja kwa moja. Mkataba wa sasa wa nyota huyo na PSG unatarajiwa kumalizika 2028.


Scott McTominay

KIUNGO wa kimataifa wa Scotland, Scott McTominay, 29, anadaiwa kusisitiza hana mazungumzo na klabu za Saudi Arabia licha ya taarifa kudai huenda akatimkia huko mwisho wa msimu. Inaelezwa kuwa McTominay ameweka akili yake yote  kuendelea kuitumikia Napoli na anafurahia maisha ndani ya viunga hivyo. Uamuzi huo pia umezirudisha nyuma timu nyingi Ulaya zilizokuwa zinahitaji saini yake.