Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magwiji wawili waangwa Real Madrid

MAGWIJI Pict

Muktasari:

  • Madrid jana ilifunga msimu kwa kishindo baada ya kuichapa Athletic Club mabao 4-2, huku staa wa Kylian Mbappe akifunga bao moja mengine yakifungwa na Brian Diaz, Jude Belligham na Gonzalo Garcia, huku wageni wakifunga kupitia kwa Garco Guzleta na Urko Uzeta.

MADRID, HISPANIA: MASHABIKI wa Real Madrid juzi waliwaaga kwa hisia kubwa wachezaji wao wapendwa, David Alaba na Dani Carvajal, katika usiku wa historia uliokuwa umejaa heshima kwenye Uwanja wa Santiago Bernabéu.

Madrid jana ilifunga msimu kwa kishindo baada ya kuichapa Athletic Club mabao 4-2, huku staa wa Kylian Mbappe akifunga bao moja mengine yakifungwa na Brian Diaz, Jude Belligham na Gonzalo Garcia, huku wageni wakifunga kupitia kwa Garco Guzleta na Urko Uzeta.

Madrid imemaliza msimu ikiwa nafasi ya pili na pointi 86 huku Athletic ikimaliza nafasi ya 12 na pointi 45.

Wakati wa tukio la kuaga mashabiki wa Madrid juzi walirudia shangwe maarufu ya Alaba ya kuinua kiti hewani, huku Carvajal akishindwa kuzuia machozi alipokuwa akiaga klabu baada ya mafanikio makubwa katika maisha yake ya soka.

MAGWI 01

Bernabéu yawaaga nyota wawili

Mashabiki wa Real Madrid walimpa Alaba heshima ya pekee katika mechi yake ya mwisho akiwa na klabu hiyo na baada ya  beki huyo wa Austria kutolewa dakika ya 68, waliinua viti juu kama kumbukumbu ya sherehe yake maarufu wakati wa ushindi wa kihistoria wa Madrid dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2022.


Alaba azungumzia kuondoka kwake kwa hisia

Alaba, ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha makubwa katika misimu ya hivi karibuni, alionekana kuguswa sana alipokuwa akitoka uwanjani. Baadaye aliwashukuru viongozi wa klabu, wafanyakazi, wachezaji wenzake na mashabiki kwa sapoti waliompa katika kipindi chake cha miaka mitano akiwa Madrid.

Akizungumza na RMTV baada ya mechi, alisema:

“Sikujiandaa sana kwa hili, hivyo hotuba itakuwa fupi. Mimi ni mtu mwenye aibu, lakini asanteni sana kwa kila kitu. Kwa kweli, nimefurahia sana miaka hii mitano pamoja nanyi. Asanteni kwa upendo na sapoti yenu. Tumepata mafanikio mengi pamoja.”

MAGWI 02

Mwisho wa enzi

Kwa upande wake, Carvajal pia alishindwa kuzuia hisia zake alipokuwa akiaga klabu aliyochezea kwa miaka mingi na kuwa mmoja wa wachezaji wenye mataji mengi zaidi katika historia yake.

Aliwashukuru viongozi, makocha, wachezaji wenzake pamoja na familia yake kwa mchango wao katika safari yake ya mafanikio.

“Usiku mwema Madridistas. Si rahisi kwangu kuzungumza kwa sababu nina hisia nyingi kutokana na namna mlivyonipenda kwaheri hii ya kipekee,” alisema Carvajal.


Amshukuru Florentino Pérez: “Yeye ndiye aliyenirudisha kutoka Ujerumani. Tumekua pamoja na kushinda mataji mengi ya Champions League. Lakini jambo kubwa zaidi ni baada ya kuumia vibaya goti, hakusita kuongeza mkataba wangu. Nashukuru sana kutoka moyoni.”


Awapongeza mashabiki Real Madrid: “Kilichopo katika uwanja huu hakiwezi kuelezeka kwa maneno; lazima ukione na ukihisi mwenyewe. Mmeendelea kunisapoti tangu siku ya kwanza hadi ya mwisho. Nataka nikumbukwe kama mtu aliyetoa kila kitu kwa ajili ya jezi hii. Jana, leo na milele. Hala Madrid!”