Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CR7 alivyopunguza pengo la mataji dhidi ya Messi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Taji hilo alilolipata wiki iliyopita na kwa kufanya hivyo amekomba la kwanza kubwa la klabu tangu Coppa Italia 2021 akiwa na Juventus, lilivutia rekodi nyingine nyuma ya ushindani na mpinzani wake wa muda mrefu, Lionel Messi.

MADRID, HISPANIA: WAKATI Cristiano Ronaldo akiwa katika msimu wake wa nne Al-Nassr, nyota huyo wa Ureno ametwaa taji lake la kwanza akiwa na klabu hiyo, likiwa ni la Ligi Kuu Saudia maarufu kama Saudi Pro League.

Taji hilo alilolipata wiki iliyopita na kwa kufanya hivyo amekomba la kwanza kubwa la klabu tangu Coppa Italia 2021 akiwa na Juventus, lilivutia rekodi nyingine nyuma ya ushindani na mpinzani wake wa muda mrefu, Lionel Messi.

Hilo sasa ni taji namba 36 kwa Ronaldo katika mashindano ya klabu na ya kimataifa kwa pamoja. Lakini, cha kushangaza hata idadi hiyo kubwa ya mataji bado inamuweka nje ya Top 10 ya wachezaji wa muda wote kwa mataji ya pamoja.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amejikuta akiwa kwenye nafasi ya pamoja ya 11 kwa muda wote na wachezaji wengine wanne, wakiwemo baadhi ya nyota aliowahi kuwa nao katika timu moja. Cristiano Ronaldo sasa yuko sawa nafasi ya 11 kwa muda wote kwa mataji ya timu aliyoshinda.

Kwa kufanya hivyo amelingana na Sergio Busquets, Angel Di Maria, Ryan Giggs na Ibrahim Hassan wote wakiwa na mataji 36. Kulikuwa na wakati ambapo kumfikia Messi ilionekana kuwa jambo linalowezekana, lakini halijawa hivyo kwa muda sasa, hasa zaidi kutokana na Ronaldo kuwa na umri wa miaka 41. Messi bado anaongoza orodha ya muda wote ya mataji kwa tofauti kubwa.

Ronaldo sasa anaweza kusema ameshinda angalau taji moja katika kila klabu aliyowahi kuchezea ikiwa ni Sporting CP, Manchester United, Real Madrid, Juventus na Al-Nassr, lakini Messi anaweza kusema vivyo hivyo pia akiwa amefanya hivyo na Barcelona, PSG na Inter Miami.

Ronaldo pia amefanikisha mambo mengi na timu ya taifa ya Ureno, akiiwezesha kushinda taji la kwanza la Euro 2016 kisha akafuata mataji ya Nations League  2019 na 2025. Kinachofuata ni Kombe la Dunia 2026, ambapo wote Ronaldo na Messi wanatarajia kuongeza taji lingine kwenye makabati yao iwapo watabeba.