Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maguire akubali msamaha wa huko Ghana

MACHESTER, ENGLAND. BEKI wa Mancheter United, Harry Maguire amekubali ombi la msamaha kutoka kwa mwanasiasa wa Ghana ambaye alimkashifu kwenye hotuba yake mwaka jana.

Mwanasiasa Isaac Adongo aling’ara kwenye vichwa vya habari mwaka jana kwa kubuni msemo wa “uchumi wa Maguire” katika hotuba ya kukosoa sera za mpinzani.

Hotuba katika bunge la taifa la Ghana ilimjumuisha akisema makamu wa rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia alifurahia kujifunga na kutoa boko kama beki huyo.

Adongo kwa mara nyingine akamuongelea Maguire baada ya miezi 12, akiangaza zaidi mabadiliko ya nyota huyo wa kimataifa wa England akimlenga mpinzani wake wa kisiasa.

“Kama unakumbuka mwaka jana nimlinganisha makamu wa rais Mahamudu Bawumia na Harry Maguire,” alisema na kumuomba radhi Maguire.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulikasirika sana nilipomtumia utetezi wako kama mfano, Maguire anaonyesha kiwango kizuri kwa sasa, amebadilika sana. Maguire anaifungia timu yake mabao kwa sasa, spika wa bunge nikueleze tu Maguire sasa ni mchezaji muhimu wa Man United.”

Beki huyo wa Man United alijibu kupitia mtandao wa kijamii kuhusu maoni ya mwanasiasa huyo: “Mbunge Issac Adongo msamaha umekubaliwa. Tuonane Old Trafford hivi karibuni.” Maguire alichapisha kwenye akaunti ya X.

Kauli ya msamaha wa Maguire imekuja baada ya mwanasiasa huyo kumkashifu akimtumia kama mfano kwenye mambo ya uchumi, kipindi hicho ambacho alikuwa anapitia wakati mgumu.

Msimu uliopita Maguire alikuwa nje ya dimba kwa muda mrefu kufuatia mwanzo mgumu wa msimu chini ya Erik ten Hag.

Lakini baada ya miezi 12, Maguire amelazimisha kurejea kwenye kikosi, akifanya vyema na kujidhihirisha kuwa mmoja wa wachezaji wachache ambao Ten Ha anawaamini kwenye safu ya ulinzi.

Maguire ameanza mechi nane za mwisho za Man United katika michuano yote kufuatia msimu mbovu na amekuwa na mchango mkubwa.

Ilifahamika beki huyo angeondoka Old Trafford dirisha la usajili la kiangazi baada ya West Ham kukubali kutoa Puauni 30 milioni, lakini uhamisho huo ulikwama kwani alionyesha nia ya kubaki na kupigania nafasi yake OT.