Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jude Bellingham kuungana na Rudiger

JUDE

Muktasari:

  • Nyota huyo wa Real Madrid anaripotiwa kuchelewesha kufanyiwa upasuaji tangu alipoumia bega kwa kuvunjika mwaka mmoja na nusu uliopita.

MADRID, HISPANIA: BAADA ya Antonio Rudiger kufanyiwa upasuaji wa goti, staa mwingine wa Real Madrid, Jude Bellingham yuko katika hatua za mwisho kufanyiwa upasuaji wa bega kutokana na tatizo la muda mrefu alilokuwa akilivumilia kwa takribani miezi 18.

Nyota huyo wa Real Madrid anaripotiwa kuchelewesha kufanyiwa upasuaji tangu alipoumia bega kwa kuvunjika mwaka mmoja na nusu uliopita.

Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Marca, inaelezwa staa huyu atafanyiwa upasuaji wa bega mara baada ya msimu huu kumalizika.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 alianguka vibaya katika mechi dhidi ya Rayo Vallecano mnamo Novemba 2023 na baada ya hapo alilazimika kukosa mechi mbili zilizofuata za Real Madrid, na pia hakushiriki mechi mbili za mwisho za kufuzu kwa Euro 2024 akiwa na timu ya taifa ya England.

Tangu wakati huo, Bellingham amekuwa akicheza huku bega lake limefungwa bandeji maalumu ili kuzuia maumivu kuongezeka.

Kulikuwa na tetesi kwamba kiungo huyo wa England angefanyiwa upasuaji baada ya Euro 2024, lakini kutokana na England kufika fainali dhidi ya Hispania, hakukuwa na muda wa kutosha wa mapumziko kabla ya msimu mpya wa LaLiga kuanza.

Bellingham alikosa wiki chache za mwanzo wa msimu huu baada ya kupata jeraha la misuli mguuni wakati wa maandalizi ya msimu, lakini aliamua kutofanyiwa upasuaji wa bega.

Upasuaji huo huenda ukasababisha asishiriki michuano ya Klabu Bingwa Dunia itakayoanza Juni 14 na kumalizika Julai 13 huko Marekani lakini bado haijathibitishwa.