Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu waangukia kwa Bruno Fernandes

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Hii inakuwa ni mara ya pili kwa matajiri hawa kutaka kumsajili Bruno baada ya kufanya hivyo katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana ambapo walikuwa tayari kutoa Pauni 80 milioni kama ada ya uhamisho na kumpa staa huyo mshahara unaofikia Pauni 600,000 kwa wiki.

AL - HILAL ya Saudi Arabia imepanga kufanya kikao kwa mara ya tatu na wawakilishi wa mchezaji wa kimataifa wa Ureno, Bruno Fernandes ili kuipata saini yake katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa matajiri hawa kutaka kumsajili Bruno baada ya kufanya hivyo katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana ambapo walikuwa tayari kutoa Pauni 80 milioni kama ada ya uhamisho na kumpa staa huyo mshahara unaofikia Pauni 600,000 kwa wiki.

Hata hivyo, kwa sasa haionekani kama dili hilo litafanikiwa kwani Bruno mwenyewe ameendelea kuonyesha nia ya kusalia Man United na hata kocha wa mashetani wekundu, Ruben Amorim ameweka wazi kwamba anataka kuona staa huyo akiendelea kuwepo.

Mkataba wa sasa wa Bruno unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu huu amecheza mechi 53 za michuano yote, amefunga mabao 19 na kutoa asisti 19.


Martin Zubimendi

KOCHA wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso anadaiwa kumjumuisha kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi kwenye orodha ya mastaa anaotaka kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa atajiunga na Real Madrid kuchukua nafasi ya kocha Carlo Ancelotti.

Hata hivyo, Zubimendi ambaye anawindwa sana na Arsenal anadaiwa kufanya makubaliano ya awali na washika mitutu hao.


Jakub Kiwior

MARSEILLE wanataka kumsajili beki wa kati wa Arsenal na timu ya taifa ya Poland, Jakub Kiwior, 25, ambaye kocha Robert de Zerbi anaamini ataenda kuboresha eneo lao la ulinzi.

Kiwior ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Arsenal hali ambayo inachangia atamani kuondoka.


Viktor Gyokeres

MKURUGENZI wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, anafanya mazungumzo kwa ajili ya kusajili mshambuliaji mpya ambapo kwa sasa amewaweka katika orodha mastaa wawili tu ambao ni Viktor Gyokeres, 26, kutoka Sporting Lisbon na mchezaji wa kimataifa wa Slovenia kutoka RB Leipzig, Benjamin Sesko, 21. Inaelezwa kigogo huyu anataka kuhakikisha mmoja kati ya wachezaji hawa anatua kwenye kikosi chao.


Leandro Trossard

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Leandro Trossard, yuko kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu mkataba mpya licha ya kupokea ofa kutoka timu mbalimbali za Saudi Arabia zinazohitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mkataba wa sasa wa Trossard unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu huu amecheza mechi 53 za michuano yote na kufunga mabao 10.


Semenyo

MABOSI wa Manchester United wanatamani zaidi kumsajili winga wa kimataifa wa  Ghana anayeichezea Bournemouth, Antoine Semenyo, 25, badala ya mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Cameroon, Bryan Mbeumo 25, kama ilivyoripotiwa hapo awali. Semenyo mwenye umri wa miaka 25, ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Bournemouth, mkataba wake wa sasa unaisha mwaka 2029.


Leroy Sane

WINGA wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Leroy Sane, hajaridhishwa na ofa ya mkataba mpya aliyopewa na Bayern Munich na huenda akaondoka kwa uhamisho wa bure mwisho wa msimu ambapo timu nyingi zimeanza kuiwania saini yake.

Anawindwa sana na Arsena, Chelsea na Barcelona.


Jonathan Tah

BEKI wa kati wa Bayer Leverkusen, Jonathan Tah, 29, ambaye anahusishwa na timu mbalimbali ikiwamo Bayern Munich na Barcelona kuelekea dirisha lijalo amesisitiza kwamba hadi sasa bado hajafanya uamuzi wa timu gani atajiunga nayo lakini atatoa uamuzi wake katika siku za hivi karibuni. Mkataba wake na Leverkusen unaisha mwisho wa msimu huu.