Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madueke anavyompima ubavu Saka Arsenal

MADUEKE Pict

Muktasari:

  • Mashabiki wa Arsenal huenda wasipende kulinganisha hilo, lakini hali hii inafanana kidogo na kipindi ambacho washambuliaji wengi walikuwa wakishindana na Harry Kane wakati wa enzi zake alipokuwa Tottenham Hotspur.

LONDON, ENGLAND: HAKUNA kazi ngumu zaidi Arsenal kuliko kugombea namba na Bukayo Saka kwenye kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta huko Emirates.

Mashabiki wa Arsenal huenda wasipende kulinganisha hilo, lakini hali hii inafanana kidogo na kipindi ambacho washambuliaji wengi walikuwa wakishindana na Harry Kane wakati wa enzi zake alipokuwa Tottenham Hotspur.

Tangu Mikel Arteta alipoteuliwa kuwa kocha zaidi ya miaka sita iliyopita, Saka amecheza mechi 40 zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote wa Arsenal.

Hivyo basi, inafaa kumpa heshima Noni Madueke, ambaye analazimika kushindana jino kwa jino na Saka, kwa Arsenal na pia timu ya taifa ya England.

Na kuna changamoto nyingine pia, Madueke na Saka ni marafiki wa karibu sana. Wawili hao wamekuwa karibu tangu utotoni baada ya kukutana kwa mara ya kwanza wakiwa kwenye akademia. Hata baba zao ni marafiki.

Lakini, Madueke hana wasiwasi kuwa urafiki wake na Saka nje ya uwanja utaathiri ushindani wao ndani ya uwanja. Kwa kweli, winga huyo anaamini uhusiano wao wa karibu unaweza kuwafanya wote wawili kuwa bora zaidi kwa klabu na taifa.

Madueke, 23, amesema: “Tunazungumza kuhusu hili muda wote. Inachekesha sana kwa sababu tuko karibu mno nje ya uwanja. Tunazungumza jinsi shinikizo la aina hiyo, kujua lazima ucheze vizuri linavyotufaa sisi sote wawili. Limekuwa zuri hadi sasa, na natumaini litaendelea hivyo.”

Katika ushindi wa Arsenal 3-2 dhidi ya Bournemouth, Jumamosi, Gabriel alisawazisha bao la mapema walilofungwa na Evanilson katika dakika ya 10, kisha Declan Rice akaipa Gunners uongozi kwa kufunga mabao mawili, huku chipukizi Eli Junior Kroupi akiwafungia Cherries bao la pili.

Lakini, Madueke pia alionyesha yuko tayari kwa changamoto ya kushindana na Saka. Wengi walinuna pale Arsenal ilipotumia Pauni 48 milioni kumsajili winga huyo kutoka Chelsea.

Hata hivyo, timu ya usajili ya klabu iliamini anaweza kuwa silaha muhimu kutokana na uwezo wake wa kuwapita mabeki. Madueke alithibitisha hilo aliposaidia kuanzishwa kwa bao la kwanza la Arsenal kupitia mbio zake za kupenya upande wa kulia. Arteta hafanyi uamuzi wa usajili kirahisi, na hufanya uchunguzi wa kina wa wachezaji.

Kwa upande wa Madueke, kocha huyo wa Arsenal alimwomba Saka kutoa maoni, kutokana na kumfahamu winga huyo kuliko wengine waliopo kwenye kikosi hicho cha Emirates.

Saka aliunga mkono usajili wa Madueke, huku Declan Rice naye akizungumza kwa sifa kubwa kuhusu mchezaji huyo kutokana na walivyokuwa pamoja timu ya taifa ya England. Kuwasili kwa Madueke kumemsaidia pia Saka, kwani sasa Arsenal wanaweza kusimamia vizuri dakika zake.

Kwa Madueke, zaidi ya mtu yeyote, ni lazima atumie kila nafasi anayopewa.