Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madrid yamkomalia Saliba

Muktasari:

  • Mabingwa hao watetezi wa Hispania wanaripotiwa kuwa na uhitaji wa kuboresha safu yao ya ulinzi inayoandamwa na majeruhi baada ya Eder Militao na David Alaba kuumia.

MADRID, HISPANIA: REAL Madrid ipo tayari kutoa pesa nyingi ili kuhakikisha inaipata saini ya beki kisiki wa Arsenal, William Saliba ambaye amependekezwa na Carlo Ancelotti tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Mabingwa hao watetezi wa Hispania wanaripotiwa kuwa na uhitaji wa kuboresha safu yao ya ulinzi inayoandamwa na majeruhi baada ya Eder Militao na David Alaba kuumia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti ya Fichajes, Madrid inafahamu kwamba itakuwa ngumu kwa Arsenal kukubali kumwachia Mfaransa huyo, hivyo inataka kuweka mpunga wa maana ambao utakuwa kama kishawishi cha suala hilo kukamilika.

Saliba amekuwa mmoja kati ya mabeki bora ndani ya England na ameisaidia sana Arsenal katika misimu mitatu iliyopita kutokana na uwezo wake.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuachana na washika mitutu hao, Saliba alisema anajisikia kama yupo nyumbani ndani ya Arsenal na haoni hilo likitokea.

“Ndiyo, bila shaka, najihisi niko nyumbani. Nilijiunga na klabu miaka mitano iliyopita lakini huu ni msimu wangu wa tatu na ninafurahia kila kitu kuanzia wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki. Najihisi nyumbani kwa hivyo, kwa nini isiwe hivyo?”

Uwezo wa Saliba umempa sifa kutoka kwa nyota wa zamani wa Arsenal na wachezaji wenzake wa timu nyingine.

Virgil van Dijk, ambaye ni mmoja kati ya mabeki bora  duniani, alikiri kuwa hakuwa katika kiwango alichonacho beki huyo alipokuwa na umri wake.

Akizungumza kwenye podikasti ya Rio Ferdinand Presents, Van Dijk alisema: “Ni wazi, Saliba anapiga hatua nzuri sana.”


“Yeye ndiye mtu wa kwanza ninayemfikiria sasa kama beki bora, anafanya vitu sahihi akiwa na mpira, anafanya kazi nzuri, nilipokuwa na umri wake, sikuwa hata karibu ya kiwango alichonacho yeye.”

Vilevile, nyota wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen aliiambia tovuti ya Arsenal mwaka jana: “Ni mchezaji mzuri. Ana kila kitu ambacho beki wa kisasa anapaswa kuwa nacho, ni mwepesi, analinda vizuri na anajua kuchezea mpira.”