Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madeni ya Man United yaongezeka kufuatia mkopo wenye riba kubwa

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa Tume ya Usalama wa Fedha na Uwekezaji Marekani (SEC), Manchester United imefanya mpango mpya wa kufadhili upya deni lake kwa kukopa Dola 500 milioni badala ya mkopo wa awali wa Dola 425 milioni.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inaweza kujikuta ikilazimika kulipa mamilioni zaidi ya pauni kila mwaka baada ya kuongeza kiwango cha mkopo wake kwa Dola 125 milioni, huku ikikubali kiwango cha juu zaidi cha riba.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa Tume ya Usalama wa Fedha na Uwekezaji Marekani (SEC), Manchester United imefanya mpango mpya wa kufadhili upya deni lake kwa kukopa Dola 500 milioni badala ya mkopo wa awali wa Dola 425 milioni.

Tofauti na mkopo wa zamani ambao ulikuwa unatarajiwa kuisha 2027 na ulikuwa na riba ya asilimia 3.79, mkopo mpya una riba ya asilimia 5.36.

Kutokana na ongezeko hilo la riba, United inaweza kulipa takribani Pauni 10 milioni zaidi kwa mwaka kama gharama za riba pekee.

Kwa mujibu wa masharti ya makubaliano hayo, klabu inaruhusiwa kutumia mkopo huo wa Dola 550 milioni kulipa deni la awali la Dola 425 milioni na pia kufadhili shughuli za kawaida za uendeshaji wa klabu.

Manchester United imeendelea kufanya marekebisho ya madeni yaliyotokana na ununuzi wa klabu uliofanywa na familia ya Glazer 2005, ambapo katika mchakato huo ilikopa fedha kwa kutumia mali za klabu kama dhamana ili kufanikisha ununuzi wake.

Kwa sasa, United inadaiwa zaidi ya Pauni 1 bilioni kupitia madeni mbalimbali, mikopo ya muda mfupi inayoweza kutumika mara kwa mara  pamoja na ada za uhamisho wa wachezaji ambazo bado inadaiwa na klabu nyingine. Hali hiyo inaongeza shinikizo la kifedha kwa klabu hiyo huku ikiendelea kutafuta njia za kuboresha matokeo yake ndani na nje ya uwanja.