Mabosi Arsenal wamchangamkia Tammy Abraham

Tuesday July 20 2021
tammy pic

ARSENAL inaangalia uwezekano wa kuipata saini ya straika wa Chelsea na England, Tammy Abraham, 23, katika dirisha hili.

Abraham ni mmoja ya wachezaji wanaowindwa sana na Tottenham na Inter Milan kwani Chelsea imeonekana kuwa haina mpango wa kuendelea kuwa naye kwa msimu ujao.
Chelsea inataka kumuuza Abraham ili kupata kiasi cha pesa inachoweza kukitumia kumsajili straika mmoja kati ya Harry Kane, 27, Romelu Lukaku, 28, au Erling Haaland katika dirisha hili.
Tammy sio mchezaji anayeonekana kuwa kwenye mipango ya Thomas Tuchel kwa msimu ujao kwani hata katika michezo ya mwisho msimu ya uliopita alikuwa hapewi nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza.

Advertisement