Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabao mawili ya Ronaldo yaibeba Al Nassr dhidi Najma

Muktasari:

  • Mchezaji huyo alirejea kwa kishindo akiifungia Al Nassr mabao mawili na mengine mawili kutoka kwa Msenegali Sadio Mane, huku moja likiwekwa wavuni na Al Hamdan na kuifanya timu hiyo kuondoka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Al Najma katika mchezo ambao kina Ronaldo walitanguliwa kwa bao la mapema.

RIYADH, SAUDI ARABIA: MSHAMBULIAJI wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo alirejea juzi kuiokoa timu yake dhidi ya aibu iliyoanza kuiandama na kuongeza matumaini sambamba na kuboresha rekodi zake katika Ligi Kuu ya nchi hiyo (Saudi Pro League).

Mchezaji huyo alirejea kwa kishindo akiifungia Al Nassr mabao mawili na mengine mawili kutoka kwa Msenegali Sadio Mane, huku moja likiwekwa wavuni na Al Hamdan na kuifanya timu hiyo kuondoka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Al Najma katika mchezo ambao kina Ronaldo walitanguliwa kwa bao la mapema.

Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or mara tano alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha ya misuli ya nyama za paja yaliyomkosesha pia mechi za timu ya taifa ya Ureno ambayo ilikwenda Marekani kwa michezo kadhaa katika mapumziko ya kalenda ya Fifa yaliyomalizika wiki hii. Hata hivyo, ushindi walioupata haukuwa rahisi kwani Al Nassr walipata wakati mgumu kutoka kwa wageni wao kwa kupata  bao la kushtukiza katika kipindi cha kwanza kabla ya mabao mawili katika muda wa nyongeza kubadili kabisa mwelekeo wa mchezo.

Al Najma walisawazisha tena dakika mbili tu baada ya kipindi cha pili kuanza, lakini Ronaldo ambaye hakuwa amecheza tangu Februari 28 alifunga penalti na kurejesha uongozi, na nyota huyo  mwenye miaka 41 aliongeza bao lingine.

Kutokana na ushindi huo, Al Nassr sasa wako juu ya msimamo wa ligi wakiwa na pengo la alama sita, huku zikiwa zimesalia mechi saba. Hata hivyo, wapinzani wao wa karibu, Al Hilal, wamecheza mechi moja pungufu. Wakati huohuo, mabao ya Ronaldo yamepunguza pengo katika orodha ya wafungaji bora huku akilenga kushinda kiatu cha dhahabu kwa mara ya tatu katika historia ya Saudi Pro League na analenga kuwa Mzungu wa kwanza kumaliza kama mfungaji bora wa ligi hiyo kwa misimu mitatu mfululizo.

Ronaldo kwa sasa yuko nyuma kwa mabao mawili dhidi ya Ivan Toney akiwa na mabao 23 katika mechi 23 za ligi msimu huu na mshambuliaji huyo anakaribia kufikisha mabao 1,000 katika maisha yake ya soka. Mabao yake mawili dhidi ya Al Najma yalikuwa ya 967 katika ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Nyota huyo anaweza kuongeza mabao watakapocheza ugenini dhidi ya Al Akhdoud Aprili 11. kisha na Al Wasl ya UAM.