Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kevin De Bruyne kumfuata Messi

KDB Pict

Muktasari:

  • Ligi Kuu ya Soka ya Marekani (MLS) inaendelea na mkakati wake wa kuvutia nyota wakubwa wa soka kutoka Ulaya ili kuongeza kiwango cha ushindani pamoja na umaarufu wa mashindano hayo duniani.

MIAMI, MAREKANI: KIUNGO Kevin De Bruyne yupo mbioni kumfuata Lionel Messi katika Ligi Kuu ya Marekani (MLS).

Ligi Kuu ya Soka ya Marekani (MLS) inaendelea na mkakati wake wa kuvutia nyota wakubwa wa soka kutoka Ulaya ili kuongeza kiwango cha ushindani pamoja na umaarufu wa mashindano hayo duniani.

Athari za usajili wa Lionel Messi na klabu ya Inter Miami zinaendelea kuonekana, huku wachezaji wengine wakubwa wakihusishwa na kuhamia Marekani.

Miongoni mwao ni Antoine Griezmann, ambaye anaripotiwa kuwa anaweza kujiunga na MLS msimu ujao ili kuipa changamoto Inter Miami.

KD 01

Mbali na majina kama Thomas Muller, Son Heung-min na Casemiro, ambaye pia amehusishwa na Inter Miami, sasa kiungo nyota wa Ubelgiji Kevin De Bruyne ameibuka kwenye rada za klabu kadhaa za MLS.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za usajili Nicolo Schira, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya soko la wachezaji, klabu mbalimbali za MLS zimeanza kufuatilia hali ya De Bruyne.

"Klabu kadhaa za MLS zimeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Napoli, De Bruyne, ambaye mustakabali wake bado hauko wazi. De Bruyne ana mkataba na Napoli hadi mwaka 2027 wenye thamani ya euro6.5 milioni kwa mwaka pamoja na bonasi, huku kukiwa na chaguo la kuuongeza hadi mwaka 2028," Schira aliandika kupitia akaunti yake ya X.

KD 02

Hii si mara ya kwanza kwa klabu za MLS kuonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34.

Kabla ya kuhamia Napoli, kulikuwa na taarifa zilizomhusisha na Chicago Fire, lakini mpango huo haukufanikiwa.

Kwa sasa, vyombo vya habari vya Italia vinaripoti kuwa De Bruyne anapanga kuendelea kubaki Napoli kwa angalau msimu mmoja zaidi na kutimiza mkataba wake wa sasa.

Kutokana na hali hiyo, Chicago Fire pamoja na klabu nyingine zinazomtaka huenda zikapaswa kusubiri hadi mwaka 2027 ili kujaribu tena kumsajili.

Aidha, Napoli inaonekana kutokuwa na mpango wa kumuuza nyota huyo kwa sasa, jambo linalopunguza uwezekano wa kuondoka kwake katika dirisha la usajili linalofuata.