Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lookman agomea mazoezi Atalanta

LOOKMAN Pict

Muktasari:

  • Hilo limekuja baada ya mkali huyo kuwashambulia kwa maneno makali mabosi wa klabu hiyo kwamba wamevunja ahadi yao waliyokuwa wamepanga juu yake.

ROME, ITALIA: WINGA, Ademola Lookman ameripotiwa kugomea mazoezi huko Atalanta ikiwa ni harakati zake za kulazimisha uhamisho wa kuachana na timu hiyo.

Hilo limekuja baada ya mkali huyo kuwashambulia kwa maneno makali mabosi wa klabu hiyo kwamba wamevunja ahadi yao waliyokuwa wamepanga juu yake.

Lookman, 27, alitoa taarifa ndefu ya kuhusu anavyojisikia kwa kile anachofanyiwa na mabosi wa timu hiyo, kwamba wangemruhusu kuondoka.

Baada ya maelezo yake hayo, staa huyo mzaliwa wa London amegomea kwenda kwenye mazoezi ya klabu hiyo ya Serie A.

Kwa mujibu wa Sky Sports ya Italia, Lookman amekosa siku mbili za mazoezi kwenye timu hiyo baada ya kuwasilisha maombi ya kutaka kuhama.

Atalanta imesisitiza kwamba haina mpango wa kumuuza Mnigeria huyo kwenye klabu nyingine ya Italia, licha ya Inter Milan kuweka ubaoni ofa ya Pauni 32 milioni kuhitaji huduma yake.

Kinachoelezwa ni kwamba Atalanta inahitaji Pauni 43.4 milioni ili kumuuza winga huyo, huku miamba mingine inayomhitaji staa huyo ni Napoli na Atletico Madrid. Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Atalanta, Luca Percassi, alisema watamruhusu Lookman kuondoka kama tu timu inayomtaka ni ya nje ya Italia.

Lookman aliibukia kutokea kwenye akademia ya Charlton kabla ya kwenda Everton, RB Leipzig, Fulham na Leicester na baadaye akatua Italia mwaka 2022.