Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lookman acharuka, agomea kuondoka Atalanta

Muktasari:

  • Staa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, ambaye pia alikuwa kwenye rada za Arsenal mwanzoni kwa dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, aliyewahi kuzichezea Charlton, Everton, Fulham na Leicester, ametamba kwa misimu mitatu huyo Italia akitokea Leipzig.

MCHEZAJI Mnigeria, Ademola Lookman amewashambulia kwa maneno makali mabosi wa Atalanta baada ya kuzuia uhamisho wake wa Pauni 39 milioni kwenda kujiunga na Inter Milan.

Staa huyo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, ambaye pia alikuwa kwenye rada za Arsenal mwanzoni kwa dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, aliyewahi kuzichezea Charlton, Everton, Fulham na Leicester, ametamba kwa misimu mitatu huyo Italia akitokea Leipzig.

Lookman, 27, ambaye alifunga hat-trick kwenye fainali ya Europa League 2024 dhidi ya Bayer Leverkusen, alisema Atalanta ilimpa ahadi kwamba atakwenda kujiunga na Inter Milan.

Na sasa staa huyo aliyechagua kuitumikia Nigeria kwenye soka la kimataifa kwa timu za wakubwa, alisema: “Natumai jambo hilo litafanywa kwa ushirikishwaji mkubwa kwa pande zote mbili kupata suluhu haraka iwezekanavyo.

“Kwa zaidi ya miaka mitatu niliyokuwa Atalanta, nimejitolea kwa kila kitu. Si tu kama mwanasoka, lakini kama binadamu pia.

"Siku zote nimekuwa nikivaa jezi hii nikiwa mwenye kujivuna kwa kuiwakilisha klabu pamoja na jiji la Bergamo, nimekuwa nikijitolea. Nilikuja hapa kwa matumaini ya kuisaidia klabu hii kupiga hatua kubwa na kutengeneza kumbukumbu za kipekee.

"Kuna klabu nyingi sana ziliifuata Atalanta kwa ajili yangu huko nyuma, lakini niliamua kubaki hapa. Lakini, nilifikia makubaliano na mmiliki wa klabu kwamba sasa ni wakati mwafaka kwa timu kupokea ofa ili waruhusu niondoke.

"Licha ya kupokea ofa ambazo naamini zilitosha kuanza majadiliano, lakini kwa bahati mbaya klabu imezuia kwa sababu ambazo sizielewi.”

Arsenal ilihitaji saini ya Lookman mapema kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kabla ya kufikiria wachezaji wengine. Inter ilipeleka ofa ya Pauni 35 milioni kwa ajili ya mchezaji hiyo, lakini ofa yao ilikataliwa.