Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yashusha pumzi kwa Isak

ISAK Pict

Muktasari:

  • Beki wa kulia, Jeremie Frimpong, naye alipata jeraha akiwa na timu ya taifa ya Uholanzi, na ana asilimia kubwa za kutocheza mechi hiyo pia.

LIVERPOOL, ENGLAND: STRAIKA wa Liverpool, Alexander Isak alirejea kwenye mazoezi kamili na kikosi hicho jana, Alhamisi, kwa mara ya kwanza mwaka huu, jambo linaloshusha pumzi kwa kocha Arne Slot, ambaye ana mechi muhimu ya FA dhidi ya Manchester City, kesho, Jumamosi.

Isak amekuwa nje ya uwanja tangu alipovunjika mfupa wa mguu katika mechi dhidi ya Tottenham Hotspur mwaka jana. Hata hivyo, licha ya kupona, Slot atachukua tahadhari katika kumrudisha mchezaji huyo, ambapo huenda ataanza kwa kucheza dakika chache akitokea benchi.

Kurudi kwake kunatoa msaada mkubwa kwa majogoo, ambao wanapambana kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao, na wanasumbuliwa na idadi kubwa ya majeruhi.

Isak alijiunga na Liverpool akitokea Newcastle United kwa ada ya rekodi ya usajili ya England ya Pauni milioni 125, lakini tangu atue amefunga mabao matatu pekee katika mechi 16 za michuano yote, ikichangiwa pia na kukaa kwake bila kufanya mazoezi rasmi na timu kwa muda mrefu kabla ya kukamilika kwa dili lake la kutua viunga vya Anfield.

Liverpool itaikosa huduma ya kipa Alisson Becker katika mechi ijayo itakayopigwa Etihad, lakini Mohamed Salah anatarajiwa kucheza baada ya kukosa mechi iliyopita kutokana na tatizo la nyama za paja.

Beki wa kulia, Jeremie Frimpong, naye alipata jeraha akiwa na timu ya taifa ya Uholanzi, na ana asilimia kubwa za kutocheza mechi hiyo pia.