Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yaonyesha uungwana kwa familia ya Jota

UUNGWANA Pict

Muktasari:

  • Jota aliyefariki katika ajali ya gari Julai, 03, 2025 akiwa pamoja na kaka yake, Andre Silva walipokuwa wanasafiri kwenda bandarini ili kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu, mkataba wake ulibakiza miaka miwili.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amethibitisha kuwa timu yake imeilipa famila ya Diogo Jota kiasi chote cha mshahara na bonasi za mkataba, ambazo alitakiwa kukipata.

Jota aliyefariki katika ajali ya gari Julai, 03, 2025 akiwa pamoja na kaka yake, Andre Silva walipokuwa wanasafiri kwenda bandarini ili kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu, mkataba wake ulibakiza miaka miwili.

Habari za kifo cha Jota ziliambatana na majonzi makubwa, huku rambirambi zikimiminika kutoka pande zote za duniani kwenda kwa familia yake hususan mkewe, Rute Cardoso.

Slot amethibitisha mabosi na wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Group (FSG), wanaendelea kulipa mkataba wa Jota kikamilifu ili kuisaidia familia yake.

"Kwa bahati mbaya tulilazimika kusajili mchezaji mmoja zaidi kuliko tulivyopanga hapo awali na ndiyo maana unaona hata matumizi yetu yalikuwa makubwa zaidi kuliko tulivyotarajia. Majonzi yaliyopo katika jiji hili ndiyo yanayofanya nijihisi faraja kuwa hapa. Nilifurahi sana kuona sapoti ya mashabiki pale jambo hili lilipotokea lakini kubwa zaidi kwa wamiliki."

UUNG 01

"Wameamua kumlipa mke wake na watoto wake pesa zote za mkataba [ni jambo la kustaajabisha]. Labda watu wanafikiri ni jambo la kawaida, lakini si kawaida katika soka. Mchezaji hayupo tena hapa lakini mabosi wameamua kuwa waungwana."

Jota alikuwa akipokea mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki ambao kwa mwaka miaka miwili ni Pauni 14.4 milioni kiasi ambacho Liverpool inadaiwa kukilipa kwa familia yake.

Mbali ya mshahara pia kuna bonasi mbalimbali ambazo hulipwa kwa timu kijumla na inaelezwa Liverpool imezijumuisha pia katika kiasi hicho.

Kijumla ripoti zinaeleza Liverpool imelipa takribani Pauni 15 milioni lakini kutokana na makato ya kodi kiasi hicho kinaweza kupungua zaidi.

UUNG 02

Mke wa staa huyu Rute alionekana pia katika sherehe za tuzo za Ballon Do'r zilizofanyika mapema wiki hii kule Paris, Ufaransa.

Baada ya kufariki Julai 03, Jota alienda kuagwa huko Ureno kabla ya kuzikwa Julai 05 na baadhi ya mastaa hawakuhudhuria ikiwemo Cristiano Ronaldo ambaye baadae ilifichuka ndiye aliyetoa gharama zote za mazishi na hakwenda ili kupunguza taharuki.