Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yajitosa kwa Gyokeres, Man United, Arsenal kazi ipo

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Wababe hao wa Anfield wanadaiwa kuingia vitani ili kupambana na Man U na Arsenal kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya  Sweden, Viktor Gyokeres, baada ya juhudi za kumpata straika wa Newcastle Alexander Isak kuonekana kugonga mwamba.

LONDON, ENGLAND: LIVERPOOL yaingia vitani na Man United na Arsenal kumnyatia Viktor Gyokeres baada ya ndoto za Alexander Isak kufifia

Wababe hao wa Anfield wanadaiwa kuingia vitani ili kupambana na Man U na Arsenal kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya  Sweden, Viktor Gyokeres, baada ya juhudi za kumpata straika wa Newcastle Alexander Isak kuonekana kugonga mwamba.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot, anataka kwa udi na uvumba kusajili mshambuliaji kabla ya kuanza kwa msimu ujao na baada ya kuona Isak imekuwa ngumu kumpata amependekeza jina la Gyokeres.

Dili la kumsajili Isak linaonekana kuwa gumu kukamilika na Newcastle ina mpango wa kumsainisha mkataba mpya ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kuwahi kutoka katika historia ya timu hiyo.

Isak kwa sasa analipwa Pauni 130,000 kwa wiki, lakini Newcastle inataka kumpandishia hadi Pauni  200,000 kwa wiki ili abaki.

Gyokeres, anayekadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 60 milioni, amefunga mabao 97 katika mechi 102 tangu ajiunge na Sporting Lisbon akitokea Coventry miaka miwili iliyopita ni miongoni mwa mastaa wanaowindwa pia na timu mbalimbali barani Ulaya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anawindwa sana na Manchester United katika dirisha hili la majira ya kiangazi lakini inadaiwa kuwa ngumu kujiunga nao kwa sababu anahitaji kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal tayari ilikataliwa ofa ya Pauni 55.3 milioni iliyoiwasilisha kwenda Sporting katika dirisha hili, lakini inatarajiwa kurudi na pendekezo jipya.

Hata hivyo, kwa saasa Gyokeres yupo katika mvutano mkali na rais wa Sporting, Frederico Varandas juu ya ada yake ya uhamisho ambapo rais huyo anataka ilipwe Euro 85 milioni jambo ambalo Gyokeres amelikataa kwani anadai kigogo huyo alimuahidi kuwa ataondoka kwa kiasi kisichozidi Pauni 30 milioni baada ya kukataa kuondoka katika dirisha lililopita la majira ya baridi.

Arne Slot anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwani Darwin Nunez yuko mbioni kujiunga na Napoli kwa ada ya Pauni 42 milioni.

Wakati huohuo, Liverpool inaendelea kumfuatilia nahodha wa Crystal Palace Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 24, na ina matumaini ya kumnasa kwa Pauni 35 milioni.

Guehi anatarajiwa kuziba nafasi ya Jarell Quansah 22, ambaye anakaribia kujiunga na Bayer Leverkusen kwa ada ya Pauni 34 milioni.