Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool, Arsenal zamtolea macho Barcola

Muktasari:

  • Winga huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na kuondoka PSG katika miezi ya hivi karibuni kutokana kukosa namba katika kikosi cha kocha Luis Enrique.

PARIS, UFARANSA: KLABU za Liverpool na Arsenal zimeaanza kupigana vikumbo kuwania saini ya nyota wa Paris Saint-Germain, Bradley Barcola.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na kuondoka PSG katika miezi ya hivi karibuni kutokana kukosa namba katika kikosi cha kocha Luis Enrique.

Kwa sasa, Barcola amekuwa nyuma ya nyota kama Ousmane Dembele, Khvicha Kvaratskhelia na Desire Doue katika safu ya ushambuliaji ya PSG.

Licha ya changamoto ya kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara, Barcola aliendelea kuonyesha kiwango kizuri katika msimu wa 2025/26.

Katika mechi 49 alizocheza katika mashindano yote, alifunga mabao 13 na kutoa pasi saba za mabao, takwimu ambazo zimevutia klabu kadhaa kubwa barani Ulaya.

Liverpool na Arsenal zote zimekuwa zikitajwa kama timu zinazoweza kumnasa mchezaji huyo.

Kwa upande wa Liverpool, Barcola anaonekana kama mmoja wa wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi ya Mohamed Salah siku za usoni.

Kwa Arsenal, anaonekana kama chaguo la kuimarisha upande wa kushoto wa ushambuliaji na kuongeza ushindani dhidi ya Gabriel Martinelli na Leandro Trossard.

Mapema wiki hii, gazeti la L'Equipe liliripoti kuwa PSG wako tayari kufikiria kumuuza Barcola baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba wake kushindwa kupata maendeleo.

Mkataba wake wa sasa unaendelea hadi mwaka 2028, lakini kutokuwepo kwa makubaliano mapya kumeongeza uwezekano wa kuondoka kwake.


Kwa Nini Anataka Kuondoka?

Kwa mujibu wa taarifa za TEAMtalk, Barcola amefikia hatua ya kuomba kuondoka PSG kwa sababu hafurahishwi na muda wake wa kucheza.

Chanzo kikubwa cha kutoridhika kwake kilitokea wakati wa mechi za Ligi ya Mabingwa.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa Barcola alisikitishwa baada ya kutopangwa kuanza katika michezo ya nusu fainali wala fainali ya mashindano hayo.

Kutotumika katika hatua hizo muhimu kulimfanya aamini kuwa itakuwa vigumu kwake kupata nafasi ya kucheza anayoamini anastahili kutokana na kiwango chake.


Arsenal au Liverpool?

Iwapo PSG wataruhusu kuondoka kwake, Arsenal na Liverpool zinaonekana kuwa miongoni mwa timu zenye nafasi kubwa zaidi ya kumpata.

Arsenal wanaweza kumpa nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha Mikel Arteta, huku Liverpool wakimwona kama mchezaji mwenye uwezo wa kuwa sehemu muhimu ya safu yao ya ushambuliaji kwa miaka mingi ijayo.

Hatma ya Barcola inatarajiwa kuwa moja ya masuala yatakayofuatiliwa kwa karibu katika dirisha la usajili la majira ya joto