Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lionel Messi ana mwaliko wa Ikulu Marekani

MESSI Pict

Muktasari:

  • Inter Miami iliifunga Vancouver Whitecaps FC mabao 3-1, Desemba mwaka jana katika Uwanja wa Chase na kutwaa taji hilo.

FLORIDA, MAREKANI: KIKOSI cha Inter Miami anachochezea Lionel Messi kinatarajia kufanya ziara katika Ikulu ya White House huko Marekani ikiwa ni miezi michache tu baada ya mpinzani wake wa muda wote Cristiano Ronaldo kwenda kukutana na Rais Donald Trump.

Timu hiyo ya Florida itatembelea jengo hilo maarufu zaidi nchini humo, Machi 5 kusherehekea ushindi wao wa Kombe la MLS.

Inter Miami iliifunga Vancouver Whitecaps FC mabao 3-1, Desemba mwaka jana katika Uwanja wa Chase na kutwaa taji hilo.

Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa klabu hiyo katika Kombe la MLS tangu ilipojiunga na mashindano hayo mwaka 2020.

Ni utamaduni kwa timu iliyoshinda ubingwa kualikwa katika Ikulu ya Rais. Columbus Crew ilikuwa timu ya mwisho ya MLS kukubali mwaliko huo mwaka 2024. Kwa mujibu wa The Athletic, afisa wa White House amethibitisha mipango hiyo.

Hata hivyo, bado haijajulikana kama Messi mwenye umri wa miaka 38 atahudhuria ziara hiyo. Mwakilishi wake hajajibu maombi ya ufafanuzi kuhusu mipango ya nyota huyo wa Argentina kuhudhuria. Inter Miami ina mchezo siku mbili baadaye dhidi ya D.C. United jijini Baltimore, umbali wa maili 53 tu kutoka White House. Iwapo atahudhuria, Messi atakuwa akifuata nyayo za mpinzani wake wa muda mrefu supastaa wa Ureno, Ronaldo, ambapo nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid CF alikutana na Rais Trump, Novemba mwaka jana.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, alihudhuria chakula cha jioni rasmi katika White House. Chakula hicho cha jioni kilifanyika siku hiyo hiyo ambayo Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman alitembelea Ofisi ya Oval.

Mmiliki wa Inter Miami, David Beckham, anaifahamu vyema ziara ya White House. Nyota huyo mstaafu alikuwa sehemu ya ujumbe uliotembelea White House baada ya kushinda Kombe la MLS mwaka 2011 akiwa na LA Galaxy. Messi alijiunga na Inter Miami mwaka 2023 baada ya kuondoka Paris Saint-Germain mwishoni mwa mkataba wake. Amechez mechi 89, akifunga mabao 77 na asisti 44.