Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi ya mabingwa Ulaya… Patachimbika

UEFA Pict

Muktasari:

  • Katika hatua hiyo ambayo, England, Ujerumani na Hispania zimefanikiwa kuingiza timu mbili mbili huku Ufaransa na Italia zikiingiza moja, michezo ya mkondo wa kwanza inatarajiwa kupigwa kuanzia April 08 na 09 na marudiano ni April 15 na 16.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya jana kumalizika kwa hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa, sasa ni rasmi kila timu imeshamtambua mpinzani wake kuelekea robo fainali ya michuano hii.

Katika hatua hiyo ambayo, England, Ujerumani na Hispania zimefanikiwa kuingiza timu mbili mbili huku Ufaransa na Italia zikiingiza moja, michezo ya mkondo wa kwanza inatarajiwa kupigwa kuanzia April 08 na 09 na marudiano ni April 15 na 16.

Miongoni mwa michezo ambayo inaonekana kusubiriwa kwa hamu ni ule wa Arsenal dhidi ya Real Madrid  ambazo kihistoria zimewahi kukutana mara mbili tu na Arsenal ndio inaonekana kuwa na rekodi nzuri.

Katika mechi hizo mbili za raundi ya 16 bora zilizopigwa msimu wa 2005/06, mchezo wa kwanza ulimalizika kwa Arsenal kushinda bao 1-0 na ule wa marudiano ukamalizika kwa sare.

Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi wa robo fainali nyingine kati ya Paris Saint-Germain na Aston Villa ambao utakuwa ni mchezo mwingine utakaovutia watu wengi.

Wababe wengine wa Hispania, Barcelona ambao wametinga hatua hii kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Benfica watakutana na Borussia Dortmund.

Timu hizi zimewahi kukutana mara tatu katika michuano hii na yote ilikuwa katika hatua ya makundi Barca ambao ni mabingwa mara.. wa michuano hii wakashinda mara mbili na mechi moja ikamalizika kwa sare.

Timu itakayopenya katika robo fainali hii itakutana na mshindi kati ya Bayern Munich na Inter Milan ambazo kabla ya mechi hii hapo nyuma zimewahi kukutana mara saba na Bayern ndio inaongoza kwa kushinda mara nyingi zaidi(04), mechi moja ikamalizika kwa sare na Inter ikashinda mbili.

Moja kati ya mechi za kuvutia zilizowahi kuzikutanisha timu hizi ni fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2009-10 ambapo Inter ilishinda kwa mabao 2-0 ambayo yote yalifungwa na Diego Milito moja kipindi cha kwanza na lingine kipindi chapili.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Villa na PSG kukutana katika michuano hii na miongoni mwa matukio yanayosubiria kwa hamu ni Marco Asensio kukutana na waajiri wake ambao wamemtoa kwa mkopo kujiunga na timu hiyo.