Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lewandowski anunua mjengo kisiwa cha raha huko Hispania

Muktasari:

  • Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 36 amekuwa akipenda kwenda likizo kwenye kisiwa hicho cha Hispania.

BARCELONA, HISPANIA: STRAIKA  wa Barcelona, Robert Lewandowski ametumia Pauni 9.2 milioni kununua jumba la kifahari huko Mallorca.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 36 amekuwa akipenda kwenda likizo kwenye kisiwa hicho cha Hispania.

Lewandowski mara kwa mara amekuwa akienda Mallorca na mkewe mrembo Anna pamoja na watoto wao wawili.

Mwaka 2021 alitumia karibu Pauni 3 milioni kwenye jumba moja huko Santa Ponca.

Kwa mujibu wa Bild, Lewandowski sasa ameamua kuongeza idadi ya nyumba zake baada ya kununua jumba hilo lenye vyumba sita huko Mallorca katika kijiji cha Camp de Mar, ambapo mjengo huo upo ufukweni. Jumba hilo lipo kwenye eneo la mita za mraba 700.

Jumba hilo lina bwawa la kuogelea pia na limejengwa kwenye eneo zuri la kuota jua. Mallorca ipo umbali wa saa moja kwa kusafiri kwa ndege kutoka Barcelona, mahali ambako Lewandowski anacheza na yupo na mkataba hadi Juni 2026.

Kabla ya hapo, Lewandowski ana jumba jingine lenye thamani ya Pauni 7 milioni huko kwao Poland kwenye jiji la Warsaw.

Mwaka jana, Lewandowski alikiri kukaribia kujiunga na Manchester United katika moja ya mahojiano yake aliposema: “Nilishafanya uamuzi kwenda Manchester United. Nakumbuka nilizungumza na Sir Alex Ferguson na nilikuwa tayari kwa hilo.

“Nilikuwa na umri wa miaka 22 au 23 pale Dortmund, Sir Alex alinipigia. Unajua huwezi kumkatalia Ferguson na kipindi hicho Man United ilikuwa moto. Nilisema sana na nilitaka kujiunga na Man United. Lakini, Dortmund ilikataa, nami nikaheshimu uamuzi huo.”