Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Leon Goretzka mambo yameiva Arsenal

Muktasari:

  • Inaelezwa Arsenal ambayo pia ilijaribu kumsajili Goretzka dirisha lililopita la majira ya baridi lakini ikaangukia pua, bado ina imani staa huyo anaweza kutua katika himaya yao.

Arsenal inaongoza katika vita ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Leon Goretzka, 31, kutoka FC Bayern Munich.

Inaelezwa Arsenal ambayo pia ilijaribu kumsajili Goretzka dirisha lililopita la majira ya baridi lakini ikaangukia pua, bado ina imani staa huyo anaweza kutua katika himaya yao.

Kocha Mikel Arteta anatajwa kuwa shabiki mkubwa wa Goretzka na anaamini ujio wake katika timu utasaidia sana kuimarisha safu ya kiungo na kuongeza uzoefu.

Goretzka alikataa mapema kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Bayern na badala yake aliwaambia wazi vigogo wa timu hiyo kuwa anahitaji kutafuta changamoto mpya.

Timu kibao za England ikiwemo Chelsea na Manchester City zimeonyesha nia ya kumsajili, lakini moyo wa Goretzka unaonekana kutamani zaidi kutua Arsenal na si kwengineko.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Goretzka amecheza jumla ya mechi 33 za michuano yote, amefunga mabao mawili na kutoa asisti moja.

Kiungo huyu atakuwa anaondoka katika viunga vya Allianz Arena baada ya kudumu kwa takribani miaka tisa akiwa mmoja kati ya mastaa waliocheza wakiwa na jezi ya miamba hiyo kwa muda mrefu.


Callum Wilson

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Callum Wilson, 34, amekubali kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na West Ham United, licha ya kuonekana kuwa karibu kuondoka katika kikosi hicho wiki chache zilizopita. Taarifa zinaeleza hatma ya Wilson West Ham ilikuwa haijulikani kwa muda, lakini pande zote mbili zimefikia makubaliano mapya yatakayombakisha mshambuliaji huyo kwa walau msimu mmoja zaidi.


Ibrahim Sangare

Manchester United imeongeza jina la kiungo wa Nottingham Forest, Ibrahim Sangare, 28, kwenye orodha ya wachezaji inaohitaji kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ripoti zinaeleza Mashetani hao Wekundu wanataka kuimarisha safu yao ya kiungo na Sangare anaonekana kuwa chaguo linalofaa kutokana na uwezo wake wa kukaba. Hata hivyo, bado haijafahamika kama ni kiasi gani Man United itawasilisha kwa Nottingham Forest, kama ofa yao ya kwanza.


Tino Livramento

Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano ya kukamilisha usajili wa beki wa Newcastle United na  England, Tino Livramento, 23, kutoka Newcastle United. Ripoti zinaeleza Man City wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi inayoonekana kupwaya kwa msimu huu na Livramento anaonekana kuwa chaguo bora kutokana na kasi yake na uwezo mkubwa wa kushambulia alionao. Hata hivyo, bado haijafahamika kama Newcastle itakubali kumwachia mchezaji huyo kirahisi.


Marcus Tavernie

Newcastle United imeonyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Bournemouth na England, Marcus Tavernier, 26, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ripoti zinaeleza Newcastle imekuwa ikiamfuatilia Tavernier kwa muda mrefu na wanaamini anaweza akavaa vyema viatu vya Sandro Tonali ambaye haonekani kuwa na asilimia nyingi za kubaki kwani vigogo wengi wanahitaji saini yake.


Sandro Tonali

REAL Madrid imewatuma maskauti wao kwenda England kwa ajili ya kumwangalia kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali, 25, ambaye kuna uwezekano ikatuma ofa ya kutaka kumsajili dirisha lijalo. Inadaiwa  maskauti wa Real Madrid walikuwepo uwanjani katika mechi ya FA Cup kati ya Newcastle na Man City  kufuatilia kiwango cha Tonali. Hata hivyo, bado haijafahamika kama Real Madrid itawasilisha ofa rasmi kwenda  Newcastle ifikapo mwisho wa msimu huu.


Julian Brandt

KIUGO mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Julian Brandt, 29,  anatarajiwa kuondoka kwenye viunga vya Signal Iduna Park mwisho wa msimu huu akiwa mchezaji huru. Mpango wa staa huyo kuondoka akiwa huru ulifikiwa baada ya benchi la ufundi kutoa ripoti ya kutohitaji aongezwa mkataba. Vilevile baadhi ya ripoti zinadai Brandt mwenyewe hakuwa anahitaji kuendelea kusalia Dortmund kwa sababu  anataka kupata changamoto mpya sehemu nyingine.


Rocco Reitz

RB Leipzig inadaiwa kufikia makubaliano binafsi na kiungo wa mkabaji wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani, Rocco Reitz, 23, na kwa sasa inafanya mazungumzo na timu yake kwa ajili ya ada ya uhamisho ili kuhakikisha dili hilo linakamilishwa mara tu baada ya dirisha la usajili kufunguliwa. Mazungumzo kati ya Leipzig na wawakilishi wa Reitz yanadaiwa yalianza tangu dirisha la majira ya baridi lakini wakati hupo hawakuwa wamefikia mwafaka.