Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bernardo Silva ni bure, kigogo Saudia atajwa

Muktasari:

  • Taarifa za kuondoka Silva zimeibuka baada ya Man City kuachana na mpango wa kuanza mazungumzo ya kumwongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo wakati ule wa sasa ukiwa umebakisha miezi michache kabla ya kutamatika.

KIUNGO wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Manchester City, Bernardo Silva, mwenye umri wa miaka 31, anatarajiwa kuondoka katika viunga vya Etihad wisho wa msimu  ambapo mkataba wake unatarajiwa kumalizika.

Taarifa za kuondoka Silva zimeibuka baada ya Man City kuachana na mpango wa kuanza mazungumzo ya kumwongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo wakati ule wa sasa ukiwa umebakisha miezi michache kabla ya kutamatika.

Ripoti zinadai  kuwa Silva, ambaye ni mchezaji muhimu katika safu ya kiungo ya Man City,  ataondoka kama mchezaji huru na kuna asilimia kubwa akatimkia moja kati ya klabu kubwa barani Ulaya ingawa kuna ofa kutoka kwa matajiri wa Al-Hilal ya Saudi Arabia ambao wapo tayari kuweka pesa nyingi mezani ili kumpata.

Kuondoka kwa Silva kunadaiwa ni sehemu ya mabadiliko ya Man City ambayo inataka kuingiza kizazi kipya baada ya kupitia nyakati ngumu katika misimu ya hivi karibuni.


Marcus Tavernier

Manchester United imeongeza jina la kiungo wa AFC Bournemouth, Marcus Tavernier, 26, katika orodha ya wachezaji inaowafuatilia dirisha lijalo la usajili. Ripoti zinaeleza Mashetani Wekundu wanaangalia uwezekano wa kuongeza nguvu katika safu ya kiungo na wanaamini Tavernier anaweza kuwa chaguo linalofaa kutokana na uwezo wake wa kushambulia. Hata hivyo, bado hakuna mazungumzo rasmi yaliyoanza kati yao.


Nick Pope

NEWCASTLE United inaripotiwa kuwa na kipaumbele cha kusajili kipa dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kiwango kibovu kilichoonyeshwa na kipa wao Nick Pope msimu huu. Newcastle pia inaonekana kutokuwa na mpango wa kufanya usajili wa moja kwa moja wa kipa wa England Aaron Ramsdale, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika kikosi chao akitokea Southampton. Kutokana na hali hiyo, Newcastle sasa inatarajiwa kuanza kutafuta kipa mpya.


Kieran Trippier

MUSTAKABALI wa mabeki wa Newcastle United, Fabian Schar na Kieran Trippier, umeanza kuwa na sintofahamu wakati huu klabu hiyo inakabiliwa na hatari ya kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao. Ripoti zinaeleza kukosa mashindano ya Ulaya kunaweza kuathiri mipango ya kikosi cha Newcastle, jambo linaloweza kusababisha baadhi ya wachezaji wakongwe kufikiria kuondoka.


Felix Nmecha

Manchester United inadaiwa kuonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund, Felix Nmecha, 25, baada ya kuona kuna ugumu kwenye kumpata Elliot Anderson. Nmecha ameivutia sana Man United kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Dortmund na amekuwa na mchango mkubwa katika safu ya kiungo. Man United inaangalia uwezekano wa kumsajili Nmecha  kama njia ya kuiongezea ubora safu ya kiungo.


Murillo

Liverpool inadaiwa kuimarisha nia yake ya kumsajili beki wa Nottingham Forest, Murillo, 23, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ripoti zinaeleza kuwa Liverpool inaamini dau la Pauni 70 milioni linaweza kutimiza usajili wa Murillo, ambaye amekuwa akionyesha kiwango bora katika safu ya ulinzi ya Forest kwa muda mrefu. Klabu hiyo ya Anfield inataka kumtumia Murillo kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi.


Andrea Cambiaso

REAL Madrid inadaiwa kuwa mstari wa mbele kuiwania saini ya beki wa pembeni wa Juventus, Andrea Cambiaso mwenye umri wa miaka 26, ambaye pia anawindwa na Arsenal na Manchester City. Mabosi wa Juventus hawaonekani kuwa tayari kumuuza staa huyu lakini mchezaji mwenyewe ameshawaambia kwamba anahitaji kuondoka kwani anaamini ni muda sahihi wa kufanya hivyo.


Marco Sensei

BARCELONA ipo katika hatua nzuri ya kumsajili beki wa kati wa Bournemouth, Marcos Senesi, 28, kwa usajili huru katika dirisha lijalo la  majira ya kiangazi na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika. Sensei amekataa kusaini mkataba mpya wa kusalia Bournemouth na badala yake amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anahitaji kuondoka kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.