Lejendi azigonganisha Chelsea, Liverpool
Muktasari:
- Cole amefichua kuwa yeye binafsi angependa pia kuona Jurgen Klopp, akiajiriwa kumrithi Maresca kwani aina ya soka lake litafaa sana katika viunga hivyo vya Stamford Bridge.
LONDON, ENGLAND: LEJENDI wa Chelsea, Joe Cole ameiingiza vitani timu hiyo dhidi ya Liverpool baada ya kuweka wazi kwamba kocha Jurgen Klopp ni mmoja kati ya wale wanaoweza kuchukua mikoba ya Enzo Maresca
Cole amefichua kuwa yeye binafsi angependa pia kuona Jurgen Klopp, akiajiriwa kumrithi Maresca kwani aina ya soka lake litafaa sana katika viunga hivyo vya Stamford Bridge.
Kwa sasa, Klopp anafanya kazi kama mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig, na Cole amedai kwamba Mjerumani huyu anafaa kumrithi Maresca ingawa kwa sasa kocha wa Strasbourg, Liam Rosenior anaonekana kuwa ndio mwenye nafasi kubwa ya kuajiriwa.
Ikiwa Chelsea itaingia kweli katika harakati za kumsajili Klopp inaweza kujikuta katika vita dhidi ya Liverpool ambayo mara kadhaa imetajwa kutaka kumrudisha kocha huyu kutokana na kiwango kibovu ambacho timu inakionyesha kwa sasa chini ya Arne Slot.
Akizungumza na tovuti ya Paddy Power, Cole amesema: "Nafahamu hili ni wazo gumu, lakini Jurgen Klopp ni chaguo sahihi, najua labda anaweza asikubali kwa sababu ni Chelsea na yeye ni Liverpool, lakini huwezi jua inatakiwa tujaribu. Ikiwa lengo kuu la klabu yako ni kushinda mataji na una mna fedha, basi inabidi uzungumze na makocha wakubwa kama yeye."
Cole pia anaamini kuwa Chelsea waliwahi sana kumwachilia Maresca ambaye alikuwa ameshinda UEFA Conference League na Kombe la Dunia la Klabu msimu uliopita.
"Makocha hawatendewi haki kabisa katika mpira wa miguu. Kuna vitu vingi vinavyomzunguka kocha. Mimi Sidhani kama alipewa muda wa kutosha. Alifanya kazi nzuri hadi siku yake ya mwisho.