Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LeBron aongoza balaa Lakers, ikiizika Rockets

Muktasari:

  • Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Toyota Center, Rockets walishindwa kabisa kuhimili presha ya mechi ya maamuzi, wakionekana kupoteza mwelekeo mapema na kushindwa kuonyesha ubora waliouonyesha katika michezo miwili iliyopita.

TEXAS, MAREKANI: MSIMU wa Houston Rockets umefikia tamati kwa maumivu makubwa baada ya kufungwa vibaya kwa pointi 98-78 dhidi ya Los Angeles Lakers katika Game 6 ya raundi ya kwanza ya mchujo katika NBA.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Toyota Center, Rockets walishindwa kabisa kuhimili presha ya mechi ya maamuzi, wakionekana kupoteza mwelekeo mapema na kushindwa kuonyesha ubora waliouonyesha katika michezo miwili iliyopita.

Baada ya kuanza vibaya mfululizo kwa kuwa nyuma 3-0, Rockets walijaribu kurudi kwa kishindo kwa kushinda michezo miwili mfululizo, lakini juhudi hizo hazikutosha kuzuia kuondolewa kwao.

LAKERS YAONYESHA UBORA

Los Angeles Lakers walionekana kuwa timu bora zaidi katika kila idara ya mchezo huo. Kuanzia mwanzo hadi mwisho, walicheza kwa umakini mkubwa, wakionyesha uzoefu na nidhamu iliyowazidi wapinzani wao.

Nyota wao LeBron James alikuwa katika kiwango cha juu, akiongoza mashambulizi na kuonyesha kwa nini bado ni mmoja wa wachezaji bora licha ya umri wake mkubwa. Alimaliza mchezo huo akiwa na pointi 28, asisti 8 na rebound 7.

Mbali na LeBron, mchango wa Rui Hachimura nao ulikuwa mkubwa katika mchezo huo, akifunga pointi 21 huku akipiga mipira mitano ya alama tatu, jambo lililoongeza pengo na kuondoa matumaini ya Rockets kurejea kwenye mchezo.

Ulinzi wa Lakers nao ulikuwa wa kiwango cha juu, wakizuia mashambulizi ya Rockets na kuwafanya washindwe kupata nafasi nzuri za kufunga.

SILAHA ROCKETS YAWAGEUKA

Mojawapo wa mambo ya kushangaza katika mchezo huo ni jinsi Rockets walivyodhibitiwa katika eneo ambalo kwa kawaida huwa nguvu yao.

Katika msimu wa kawaida, Rockets walikuwa miongoni mwa timu bora katika kuchukua rebounds, lakini katika mchezo huu walizidiwa kabisa. Lakers walionekana kuwa na njaa zaidi ya mipira ya pili, wakichukua rebounds muhimu za kushambulia na kujenga nafasi nyingine za kufunga.

Kwa takwimu, Lakers walimaliza wakiwa na rebounds 54 dhidi ya 45 za Rockets, huku wakiongoza pia katika offensive rebounds, yaani kuokota tena mpira uliokosa kuingia kapuni ukiwa unashambulia.

Hali hiyo iliwapa faida kubwa kwani walipata nafasi nyingi zaidi za kupiga na kuongeza pointi. Hata wachezaji ambao hawakutarajiwa, kama Luke Kennard, walijitokeza kuchukua rebounds muhimu, jambo lililoonyesha wazi tofauti ya juhudi kati ya timu hizo mbili.


HIKI KILIWAGHARIMU

Tatizo kubwa zaidi kwa Rockets lilikuwa ni kushindwa kufunga. Kuanzia mwanzo wa mchezo, walionekana kukosa makali ya kushambulia, wakifunga pointi chache sana na kukosa mipira rahisi.

Katika robo ya kwanza walifunga pointi 18 pekee, huku katika robo ya pili wakifanya vibaya zaidi kwa kufunga pointi 13. Hadi mapumziko ya nusu mchezo, walikuwa na pointi 31 pekee, takwimu duni sana kwa mchezo wa kiwango hicho.

Kulikuwa na kipindi kibaya zaidi ambapo Rockets walikaa kwa dakika tano bila kufunga hata pointi moja, hali iliyoipa Lakers nafasi ya kukimbia na kujenga uongozi mkubwa. Wachezaji wao walishindwa kutumia nafasi walizopata, wakipiga kwa asilimia ndogo sana. Kwa ujumla, walipiga kwa asilimia 35 pekee ya mafanikio, huku mipira ya alama tatu ikiwa tatizo kubwa zaidi.

Majina kama Jabari Smith Jr. na Reed Sheppard hayakuweza kuleta tofauti kama ilivyotarajiwa, huku wakikosa mipira mingi muhimu.

Zaidi ya hayo, makosa ya kupoteza mipira (turnovers) yaliwapa Lakers nafasi nyingi za kushambulia, jambo lililozidi kuwaumiza.

Kwa Rockets, huu ni mwisho mchungu wa msimu ambao ulikuwa na matumaini makubwa. Vijana wao walionyesha dalili nzuri za ukuaji, lakini uzoefu na ubora wa Lakers uliamua matokeo ya mwisho. Kwa upande wa Los Angeles Lakers, ushindi huu unaonyesha kuwa bado ni timu yenye uwezo mkubwa wa kufanya vizuri katika mchujo, hasa wanapokuwa na kiongozi kama LeBron James.