Kwa kiwango kile? hawatoboi kwa Brighton

MANCHESTER, ENGLAND. MKONGWE wa Manchester United, Roy Keane amewachana mastaa wa timu hiyo kufuatia kiwango kbovu walichoonyesha kwenye robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Fulham uliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford.

Licha ya kuboronga kwenye mchezo huo Man United iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, na kutinga nusu fainali ambayo itamenyana na Brighton katika uwanja wa Wembley.

Aidha Keane akasisitiza alipoteza matumaini kuelekea mashindano hayo akidai endapo wachezaji wa Man United hawatakuwa makini Brighton itawafunga kwenye mechi ya musu fainali.

Man United ilisawazisha bao kupitia mkwaju wa penalti ambayo ilifungwa na Bruno Fernandes baada ya kuwa nyuma kwa bao moja dhidi ya Fulham iliyokuwa pungufu, aidha timu hiyo ikawa pungufu baada ya wachezaji wao wawili kulimwa kadi nyekundu.

Aleksandar Mitrovic alipachika bao kwa upande wa Fulham kipindi cha pili, lakini cha kushangaza mchezaji huyo akalimwa kadi nyekundu baada ya kumzonga refa Chris Kavanagh, baada ya kuamuru mkwaju wa penalti dhidi yao baada ya Willian kugusa mpira akimzuia Jadon Sancho asipachike bao kwenye nyavu.

Licha ya ushindi huo, Keane alikiri kuwa hakufurahishwa na kiwango waliionyesha Man United akisisitiza hata Ten Hag amesisikitishwa.

"Lengo la mashindano ya Kombe la FA ni kutinga raundi zinazofuata, nadhani Ten Hag amesikitishwa sana na alichoona, ni kweli Fulham ina uzoefu, lakini kwa upande wa Man United walicheza hovyo, nilipoteza matumaini kabisa, tabia hii imejirudia kila mara, wachezaji wanajisahau wakidhani kwamba wana uwezo wa kushinda mechi kila siku, kama watacheza chini ya kiwango kwenye mechi ya nusu fainali Brighton itawafunga," alisema Keane

Fulham ilikuwa imara dakika zote za mchezo dhidi ya Man United lakini iwakaruhusu mashetani wekundu kurejea mchezoni, Bruno Fernandes na Marcel Sabitzer wakainusuru timu yao na kutinga nusu fainali.

Sasa Man United itacheza nusu fainali ya Kombe la FA na na robo fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Sevilla na Brighton, mechi hizi zinatarajiwa kucheza mwezi ujao, lakini kwanza itarejea dimbani kucheza mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcasle baada ya mapumziko kwaajili ya mechi za kimataifa.