Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha amorim kung’atuka atoa sababu nzito Man United

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Man United, Jumapili ilikumbana na kipigo cha 17 kwenye Ligi Kuu England msimu huu, wakati ilipokubali kuchapwa 2-0 na West Ham United uwanjani Old Trafford.
no

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amefichua kwamba atamwaga manyanga ya kuinoa timu hiyo kama atashindwa kubadilisha kiwango cha timu hiyo ndani ya uwanja.

Man United, Jumapili ilikumbana na kipigo cha 17 kwenye Ligi Kuu England msimu huu, wakati ilipokubali kuchapwa 2-0 na West Ham United uwanjani Old Trafford.

Kipigo hicho kimefanya Man United kucheza mechi saba bila ya kushinda kwenye Ligi Kuu England, ikitoka sare mbili na vichapo vitano - ikiwa ni muda mrefu zaidi kwenye michuano hiyo tangu 1992.

Na sasa, timu hiyo iliyotinga fainali ya Europa League imeshika hadi nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi baada ya mabao ya Tomas Soucek na Jarrod Bowen wa West Ham na kupanda kwenye msimamo.

Kocha Amorim alionekana kuhuzunishwa baada ya mechi kumalizika na alifichua atakuwa tayari kung’atuka kama atashindwa kubadili hali ya mambo kwenye timu hiyo.

Amorim, 40, alisema: “Sitaki kuzungumzia wachezaji. Nataka kujizungumzia mwenyewe na utamaduni wa klabu na utamaduni wa timu. Hilo ndilo ninalolifikiria. Tunahitaji kubadili hili, tunahitaji kuwa na nguvu kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Kwa sababu hatuwezi kuwa na msimu kama huu mwakani. Kama hilo litaendelea, tutaacha nafasi kwa ajili ya watu wengine.

“Linanigusa. Sio kosa la wachezaji, ni kosa langu, nawajibika. Kama tunashindwa kubadili mambo, tutaachia hii nafasi kwa watu wengine.”

Man United imekumbana na kipigo cha tisa kwenye Ligi Kuu England katika mechi ya nyumbani msimu huu, ikiwa ni vipigo vingi zaidi kwa msimu mmoja ambavyo iliwahi kutokea pia kwenye misimu ya 1930/31, 1933/34, na 1962/63.

Man United imejikuta ikiwa nyuma 1-0 kwa mara ya 12 uwanjani Old Trafford msimu huu, huku ni Leicester City tu (15) ndiyo iliyoongozwa mara nyingi zaidi kwenye mechi za nyumbani msimu huu.

Amorim alisema: “Hatuchezi vizuri sana kwenye Europa League, lakini kuna hisia tofauti. Ni kitu tunachopaswa kukifanyia kazi ndani na nje ya uwanja. Kama tutashindwa kufanya hivyo, tutaondoka tutatoa nafasi kwa watu tofauti. Tunakwenda kucheza na timu ya Ligi Kuu England kwenye fainali, hivyo mechi itakwenda kuwa ngumu. Kwangu mimi ishu sio kushinda Europa League kwa sababu tatizo ni kubwa zaidi ya hilo. Tumepoteza hisia kwamba sisi ni klabu kubwa.”