Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa hili...! Gyokeres ana kazi ya kufanya

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Arsenal na Liverpool zilishindwa kufungana baada ya kutoka 0-0 uwanjani Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika usiku wa Alhamisi.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA wa Arsenal, Viktor Gyokeres amekuwa gumzo baada ya kutoka kapa kwenye mechi ya Liverpool, huku takwimu zake za uwanjani zikizua mjadala.

Arsenal na Liverpool zilishindwa kufungana baada ya kutoka 0-0 uwanjani Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika usiku wa Alhamisi.

Matokeo hayo yaliifanya Arsenal ya kocha Mikel Arteta kushindwa kuweka pengo la pointi kufikia nane kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo.

Lakini, gumzo kubwa lilikuwa straika wa Pauni 63.5 milioni, Gyokeres, ambaye alisajiliwa na Arsenal kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi ikiaminika atakuja kumaliza tatizo la kufunga mabao lililokuwa likiandama timu hiyo ya Emirates.

Licha ya kwamba wachezaji wengine wa Arsenal walishindwa kuonyesha viwango bora, lakini staa huyo anayevaa jezi Namba 14, hali yake ilikuwa mbaya zaidi.

Katika usiku ambazo Arsenal ilihitaji ushindi muhimu nyumbani, Gyokeres aligusa mpira mara nane tu uwanjani, huku moja ya matukio yake ya kugusa mpira ni wakati wa kuanzisha mechi.

Na wakati alipotolewa uwanjani kwenye dakika 64 kumpisha Mbrazili Gabriel Jesus, mashabiki waliona ni heri maana walikuwa wamesahau kama straika huyo wa Sweden alikuwamo uwanjani. Na mashabiki wachache walisikika wakimzomea staa huyo wa zamani wa Coventry wakati alipokuwa akitolewa uwanjani.

Gary Neville, ambaye alikuwa mtangazaji mwenza wa mechi hiyo, amesema: “Haishangazi. Gyokeres hakuwa na kitu chochote kwa usiku wote. Hakuwa akipata huduma na hakuna kingine alichofanya kujihusisha na mchezo, anapaswa kupambana.”

Gyokeres amefunga mabao matano kwenye mechi 19 alizochezea Ligi Kuu England msimu huu. Mabao mawili kati ya hayo alifunga dhidi ya Leeds United, Agosti mwaka jana, huku mengine alifunga dhidi ya Nottingham Forest, Burnley na Everton.

Straika huyo amefunga mabao mawili mengine kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini, bao lake la karibu alilofunga kwa njia ya kawaida alifunga Novemba 1.

Gabriel Jesus amerudi uwanjani siku za karibuni baada ya kuwa nje kwa muda mrefu, huku Kai Havertz naye akiwa kwenye hatua za mwisho kuanza kucheza.

Lakini, kocha Arteta haamini kwamba kurudi kwa wachezaji hao kunaweza kumpa wakati mgumu straika Gyokeres.