Gwiji England amshauri Viktor Gyokeres
Muktasari:
- Mtangazaji huyo wa zamani wa kipindi cha Match of the Day, Lineker amesema amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana straika huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 64 milioni kwenda kuongeza makali kwenye fowadi ya miamba hiyo ya Emirates.
LONDON, ENGLAND: GARY Lineker amemtaka straika wa Arsenal, Viktor Gyokeres kujifunza kwa Dominic Calvert-Lewin wakati huu akiendelea kuzoea mazingira ya Ligi Kuu England.
Mtangazaji huyo wa zamani wa kipindi cha Match of the Day, Lineker amesema amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana straika huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 64 milioni kwenda kuongeza makali kwenye fowadi ya miamba hiyo ya Emirates.
Gyokeres, 27, amefunga mabao matano kwenye Ligi Kuu England kabla ya mechi ya Jumanne dhidi ya Aston Villa na amefunga mara mbili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini, staa huyo wa kimataifa wa Sweden si tishio kwenye kufunga mabao kama mashabiki walivyokuwa wakiamini, kutokana na kile alichofanya wakati alipokuwa Sporting Lisbon msimu uliopita, mabao 54 katika mechi 52.
Straika wa Leeds United, Calvert-Lewin, kwa sasa amekuwa kwenye kiwango bora katika Ligi Kuu England, akifunga mabao manane na ametikisa nyavu katika kila mechi ya mechi sita zilizopita. Na Lineker anaamini Calvert-Lewin ni mfano mzuri wa kuonyesha kile ambacho straika anapaswa kufanya baada ya kufunga bao dhidi ya Sunderland, Jumapili iliyopita.
Lineker amesema: “Nimekuwa nikimtazama Gyokeres kwa ukaribu sana kwa wiki za karibuni, nadhani ni mmoja wa mastraika wazuri. Ni mtu ambaye amekuwa akisubiri mpira, hadi ufike ndipo akashambulie kwenye nafasi. Hicho ndicho mabeki wanafanya, yeye anapaswa kuwa kama mcheza kamari hivyo, akisie eneo ambalo mpira utakwenda na kuwahi kwenye eneo.
“Unahitaji kuwaibia hatua mabeki, lakini yeye hafanyi..”