Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kura kuamua hatima ya Rashford Barcelona

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo Mwingereza kwa sasa anaichezea Barcelona kwa mkopo akitokea Manchester United kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.

BARCELONA, HISPANIA: NOMA sana. Mashabiki wa Barcelona wamepiga kura kuamua kama mshambuliaji Marcus Rashford asajiliwe jumla au miamba hiyo ya Nou Camp aiachane naye tu aondoke mkopo wake ukimalizika.

Fowadi huyo Mwingereza kwa sasa anaichezea Barcelona kwa mkopo akitokea Manchester United kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Rashford, 28, amekuwa na kiwango bora tangu alipotua Hispania na amekuwa panga pangua kwenye kikosi cha Hansi Flick. Amecheza mechi 24 za michuano yote katika kikosi cha Barca msimu huu, akifunga mabao saba na kuasisti 11.

Kiwango chake kimevutia mashabiki na hilo ndilo lililoonekana kutokana na zoezi la upigaji kura lililoendeeshwa na Mundo Deportivo, ambapo asilimia 54.6 ya kura hizo za mashabiki wa Barca waliwataka mabosi wao wakifanyie kazi kipengele cha kumbeba jumla mchezaji huyo.

Barcelona inaweza kumchukua Rashford kwa ada ya Pauni 26 milioni mwishoni mwa msimu. Hata hivyo, kuna kura zaidi ya theluthi moja zimegomea usajili wa mshambuliaji huyo, asibebwe jumla, huku asilimia 6.3 ya kura zinataka mabosi wa timu hiyo wasubiri kwanza hadi msimu umalizike, ili waone kama kiwango chake kinastahili kumbakisha.

Rashford amekuwa panga pangua kwenye kikosi cha Barcelona tangu alipotua, akikosa mechi moja tu alipokuwa na homa.

Kura hizo za mashabiki zitampa mwanga kocha Flick kuona umuhimu wa kubaki au kutokubaki na mchezaji huyo.