Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuna timu Ujerumani inamtaka Xabi Alonso

Muktasari:

  • Alonso alitimuliwa na Madrid baada ya mechi 34 na miezi sita tu akiwa kocha mkuu katika Uwanja wa Bernabeu.

MADRID, HISPANIA: XABI Alonso inaripotiwa kufikiwa kwa ajili ya kurejea kwenye kazi ya ukocha, ikiwa ni wiki moja baada ya kufukuzwa na Real Madrid.

Alonso alitimuliwa na Madrid baada ya mechi 34 na miezi sita tu akiwa kocha mkuu katika Uwanja wa Bernabeu.

Sasa, kwa mujibu wa gazeti la BILD, kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 tayari yuko kwenye mazungumzo ya kurejea kufundisha klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani.

Inadaiwa viongozi wa Frankfurt tayari wamewasiliana na Alonso kuhusu uwezekano wa kuchukua mikoba ya ukocha katika klabu hiyo. Haya yanajiri baada ya Frankfurt kumfuta kazi kocha wao, Dino Toppmoller kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya yaliyoiacha timu hiyo katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Bundesliga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Eintracht, Markus Krosche, aliripotiwa kuwa na nia kubwa ya kukutana na Alonso, ambaye kwa sasa yuko likizo baada ya kupoteza kazi yake Madrid. Alonso bado anaheshimika sana Ujerumani kutokana na kazi yake ya awali akiwa kocha wa Bayer Leverkusen.

Katika msimu wake wa kwanza na Leverkusen, Alonso aliiongoza klabu hiyo kushinda mataji mawili ya ndani bila kupoteza mechi hata moja na kufika fainali ya Europa League walikoteza dhidi ya Atalanta ya Italia.

Alonso pia amehusishwa na kazi nyingine kadhaa, ikiwemo Tottenham na Manchester United. Kwa upande mwingine, Real Madrid bado wanaendelea kumtafuta kocha wa kudumu kuchukua nafasi ya Alonso, baada ya kocha wa mpito Alvaro Arbeloa kuanza vibaya kazi hiyo.

Timu ya Arbeloa ilitolewa kwenye michuano ya Copa del Rey na timu ya daraja la pili, Albacete, baada ya kufungwa mabao 3-2 katika kipigo cha aibu.

Hata hivyo, beki huyo wa zamani aliyeustaafu aliiongoza Madrid kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Levante kwenye LaLiga mwishoni mwa wiki hii.