Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuna swali? Lakers bila LeBron James

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Lakers, LeBron, 40, atakosa angalau katika michezo mitano ya mwanzo ya msimu na atapimwa tena baada ya wiki tatu hadi nne ili kujua maendeleo yake.

CALIFORNIA, MAREKANI: LOS Angeles Lakers imejikuta kwenye wakati mgumu kuelekea mwanzo wa msimu mpya wa NBA 2025/26, baada ya kuthibitishwa kuwa nyota wa timu hiyo LeBron James hatakuwepo kwenye michezo ya awali kutokana na majeraha.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Lakers, LeBron, 40, atakosa angalau katika michezo mitano ya mwanzo ya msimu na atapimwa tena baada ya wiki tatu hadi nne ili kujua maendeleo yake.

LeBron amepata shida kwenye neva. Shida hiyo ilikuwa ikimsumbua tangu mwishoni mwa msimu uliopita na ndiyo maana amekuwa akihisi maumivu yanayosambaa kutoka eneo la kiuno kushuka hadi miguuni.

Kocha mpya wa Lakers, JJ Redick amesema wanalazimika kukabiliana na hali hiyo kwa kuandaa mbinu mbadala.

“Tunahitaji kucheza kwa karata tulizo nazo. Ni ukweli mchungu, lakini hatuwezi kubadili hali. LeBron anaendelea na programu yake binafsi ya kurejea kwenye hali nzuri,” anasema Redick.

LeBron hajashiriki mazoezi ya pamoja tangu kambi ya mazoezi ilipoanza wiki iliyopita na pia amekosa michezo yote ya awali ya maandalizi. Hali hiyo inamaanisha kwamba Lakers wataanza msimu bila kiongozi wao uwanjani, jambo linaloleta changamoto kiufundi.

Msimu uliopita LeBron alikuwa katika kiwango cha juu licha ya umri wake mkubwa. Alimaliza akiwa na wastani wa kufunga pointi 25.2 kwa mchezo, asisti 7.9 na rebaundi 7.1 huku akitupa mitupio kwa usahihi wa asilimia 52.6.  Zaidi ya takwimu hizo, LeBron ndiye injini ya mfumo wa Lakers. Kukosekana kwake kutakuwa na athari katika sehemu ya mashambulizi ya Lakers. Bila uwepo wake jukumu hilo litamwangukia Luka Doncic ambaye anaingia msimu wake wa pili ndani ya timu hiyo.

Doncic ni mchezaji mwenye kipaji na uwezo wa kubeba timu, lakini anahitaji muda wa kuwa na muunganiko na wachezaji wenzake.

Redick atalazimika kumruhusu Luka kuwa huru zaidi katika kupanga mashambulizi huku Deandre Ayton akibeba majukumu mengine. Katika michezo ambayo LeBron atakosa, Lakers wanakabiliwa na ratiba ngumu ikiwemo mchezo wa ufunguzi dhidi ya Golden State Warriors na michezo mingine saba ndani ya siku 13.

Bila LeBron, Redick atalazimika kubadili mbinu na kutumia kikosi kipana zaidi ili kudhibiti uchovu wa wachezaji.

Hata hivyo, kipindi hiki kinaweza pia kuwa fursa kwa wachezaji vijana kama Austin Reaves, Max Christie na hata Rui Hachimura kuonyesha thamani zao. Hawa wana nafasi ya kujitokeza na kusaidia kuziba pengo la muda la nahodha wao.

Kwa upande wa kiufundi, Redick ataweka presha kubwa kwa Redick na Ayton kujenga ushirikiano baina yao mapema. Ikiwa watapata muunganiko mzuri nzuri, Lakers wanaweza kutoboa bila ya kuwa na LeBron.

Katika mazoezi ya hivi karibuni Redick ameanza kushiriki mazoezi ya pamoja huku Ayton akionekana kuwa katika hali nzuri. “Tunahitaji kuzoeana zaidi kama timu,” anasema Ayton.

“Nimekuwa nikisubiri kucheza na LeBron na Luka kwa pamoja, lakini kwa sasa tunajipanga na hali tuliyonayo.”

LeBron amekuwa akisafiri na timu katika michezo ya maandalizi akifanya mazoezi binafsi kwa nia ya kurejea haraka. Kwa sasa Lakers wanatumaini matibabu na mazoezi maalumu anayofanya yatamrudisha uwanjani mwishoni mwa Oktoba au mwanzoni mwa Novemba.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa NBA, kumtegemea Doncic peke yake bila LeBron kunaweza kuwa hatari hasa katika michezo migumu na yenye ushindani dhidi ya timu zenye wachezaji hatari hasa kwenye safu zao za ushambuliaji kama Phoenix Suns na Denver Nuggets.

LeBron amekuwa akisafiri na timu katika michezo ya maandalizi, akifanya mazoezi binafsi kwa nia ya kurejea haraka. Mashabiki waliingiwa hofu wiki hii baada ya kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, ambao baadaye ilibainika ni tangazo la kinywaji cha konyagi. Kwa sasa, Lakers wanatumai kwamba matibabu na mazoezi maalum anayofanya yatamrudisha uwanjani mwishoni mwa Oktoba au mwanzoni mwa Novemba. Redick amesisitiza kwamba hatamharakisha kurejea, akisema: “Tunamhitaji akiwa kamili.”

Kwa mujibu wa wachambuzi wa NBA kutegemea Doncic pekee bila LeBron kunaweza kuwa hatari hasa katika michezo migumu na yenye ushindani dhidi ya timu zenye wachezaji hatari hasa kwenye safu za ushambuliaji ikiwamo Phoenix Suns na Denver Nuggets.

Hata hivyo, Lakers wana imani kubwa kwamba nguvu mpya za Ayton zitasaidia kupunguza madhara.

LeBron amekuwa akisafiri na timu katika michezo ya maandalizi, akifanya mazoezi binafsi kwa nia ya kurejea haraka. Mashabiki waliingiwa hofu wiki hii baada ya kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii ambao baadaye ilibainika ni tangazo la kinywaji cha konyagi.

Kwa sasa, Lakers wanatumai kwamba matibabu na mazoezi maalum anayofanya yatamrudisha uwanjani mwishoni mwa Oktoba au mwanzoni mwa Novemba. Redick amesisitiza kwamba hatamharakisha kurejea, akisema, “Tunamhitaji akiwa kamili.”

Kwa mujibu wa wachambuzi wa NBA, kutegemea Doncic peke yake bila LeBron kunaweza kuwa hatari hasa katika michezo migumu na yenye ushindani mkali dhidi ya timu zenye wachezaji hatari hasa kwenye safu zao za ushambuliaji kama Phoenix Suns na Denver Nuggets.

Hata hivyo, Lakers wana imani kubwa kwamba nguvu mpya za Ayton zitasaidia kupunguza madhara.