Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Ronaldhinho bado wamo

Gaucho Pict
Gaucho Pict

Muktasari:

  • Ronaldhinho aliyewahi kuichezea Barcelona kwa sasa ana miaka 44, lakini namna alivyocheza pamoja na wakongwe wenzake katika mechi hiyo iliyopewa jina la 'Legends of El Clasico' ilikuwa ni shoo bab'kubwa iliyovuta hisia za mamilioni ya watazamaji waliofuatilia mchezo huo kupitia televisheni duniani kote.

DOHA, QATAR: MIAKA tisa baada ya kuachana na soka la ushindani, Ronaldhinho Gaucho kacheza mechi yake ya tatu ya maonyesho iliyohusisha mastaa wa zamani waliowahi kuichezea Barcelona na Real Madrid mjini Doha, lakini alivyoupiga ni kana kwamba ni kijana wa miaka 20.

Ronaldhinho aliyewahi kuichezea Barcelona kwa sasa ana miaka 44, lakini namna alivyocheza pamoja na wakongwe wenzake katika mechi hiyo iliyopewa jina la 'Legends of El Clasico' ilikuwa ni shoo bab'kubwa iliyovuta hisia za mamilioni ya watazamaji waliofuatilia mchezo huo kupitia televisheni duniani kote.

Mchezo huo ulimalizika kwa Barcelona kushinda kwa penalti baada ya wababe hao kumaliza dakika 90 wakiwa wamefungana kwa mabao 2-2.

Lakini, mchezo huo ulioshuhudiwa uwanjani na zaidi ya mashabiki 31,000, ambapo ulishuhudia zaidi shoo ya Ronaldhinho akipiga zile chenga za maudhi za enzi zake na kuwaacha mashabiki vinywa wazi, ilhali pia kasi yake ikiwa ya juu katika ukokotaji mpira.

Bao lake la pili la mpira wa moja kwa moja kutoka zaidi ya mita 30 katika dakika ya 16 lilitinga nyavuni likitokana na kujipinda kupiga mpira uliozunguka ukuta wa wachezaji wa Real Madrid.

GAU03
GAU03

Wakati akipiga mpira huo, Ronaldhinho alirudi hatua tatu nyuma kisha alipiga mpira ulioenda moja kwa moja wavuni kwenye kona ya juu.

Mchezaji huyo bora wa dunia 2005, aliendelea kusimamia shoo upande wa Barcelona na alikuwa mwiba kwa safu ya kiungo ya Madrid iliyokuwa chini ya wakongwe Luis Figo na Clarence Seedorf.

Kwa jumla, Ronaldinho aliichezea Barcelona mechi 207 akijiunga na timu hiyo 2003 kutokea PSG na kuondoka 2008 kwenda AC Milan. Aliifungia mabao 94, akiwa na asisti 71. Pia aliichezea Brazil mara 97 akishinda Kombe la Dunia 2002.

Mapema katika dakika ya nane Juan Pablo Sorin aliitanguza Barcelona kwa bao la kuongoza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Ludovic Giuly ambaye Julai 10, mwaka huu, alisherehekea miaka 48 ya kuzaliwa.

GAU02
GAU02

Sorin, aliyecheza Barcelona kwa miezi sita 2003, aliambaa na mpira katika winga ya kushoto na kutoa pasi kwa mfungaji aliyeutumbukiza mpira wavuni kwa ustadi mkubwa uliomuacha kipa wa Madrid, Francisco Buyo mwenye umri wa miaka 66 akishangaa.

Kuna wakati Barcelona walioongoza kwa mabao 2-0 na ilionekana kana kwamba wangeshinda mchezo huo, lakini hawakufunga tena na kuwafanya Madrid kusawazisha kupitia kwa Figo ambaye pia alichezea Barcelona katika maisha yake ya soka dakika ya 60 na Edwin Congo aliyefunga dakika nne baadaye na mechi kumalizika kwa mabao 2-2, huku mikwaju ya penalti ikiamua ushindi.

Katika mikwaju ya penalti, Frank de Boer alikosa kwa Barcelona, lakini kipa wa timu hiyo, Jesus Angoy aliokoa mikwaju ya Congo na Jose Amavisca.

Hata hivyo, malejendi wa Barçelona walikuwa moto wakati wote wa mchezo na Ricardo Quaresma na David Villa waliokuwa wakitambaa kushoto na kulia walifanya kazi kubwa kupandisha mashambulizi kupitia pembeni.

GAU01
GAU01

Timu hiyo ilipata penalti mapema tu baada ya Quaresma kukwatuliwa ndani ya eneo la hatari, lakini Patrick Kluivert alishindwa kuukwamisha mpira wavuni kwani kipa wa Madrid, Pedro Contreras alipangua mpira na kuishia kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.


Real Madrid: Buyo; Núñez, Pavón, Fernando Sanz, Raúl Bravo; Milla, Seedorf, Figo, Savio, Amavisca; Congo. Pia wengine waliocheza ni Contreras, Julio Llorente, Iván Campo, Agus, Júlio Baptista, Munitis and Álvaro Mejía.


Barçelona: Vítor Baía; Fernando Navarro, De Boer, Abidal, Sorín; Trashorras, Mendieta; Giuly, Rivaldo, Ronaldinho; Villa. Also played – Angoy, Déhu, Kluivert, Roger García, Jofre, Sergi and Quaresma.