Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Mane kawapa Liverpool kiungo mkali

Muktasari:

  • Staa huyo wa Kidachi alijiunga na Bayern akitokea Ajax kwenye dirisha moja la majira ya kiangazi ambalo alishuhudiwa pia Mane, akiondoka Liverpool kwenda kukipiga huko Allianz Arena mwaka 2022

LIVERPOOL, ENGLAND: KIUNGO, Ryan Gravenberch amekiri kwamba staa wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane ndiye aliyemshawishi kuhama kutoka Bayern Munich kwenda kukipiga Anfield mwaka 2023.

Staa huyo wa Kidachi alijiunga na Bayern akitokea Ajax kwenye dirisha moja la majira ya kiangazi ambalo alishuhudiwa pia Mane, akiondoka Liverpool kwenda kukipiga huko Allianz Arena mwaka 2022. Na licha ya kuiwezesha Bayern kushinda ubingwa wa Bundesliga, wachezaji hao wawili hawakuwa na wakati mzuri sana katika kikosi hicho cha Ujerumani, ambapo kwa pamoja wamecheza mechi 19.

Gravenberch alianza mechi sita kati ya 34 kwenye kikosi cha Bayern kabla ya kutimkia zake Liverpool kwa dili la Pauni 40 milioni kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka 2023. Kwa upande wa Mane alicheza mechi 38, akifunga mabao 12 na kuasisti mara sita, lakini alionekana kuwa ni mchezaji wa ziada chini ya kocha Thomas Tuchel, ambaye kwa sasa ndiye kocha wa timu ya taifa ya England.

Supastaa huyo wa Senegal kwa sasa anakipiga Al Nassr huko Saudi Arabia, alikojiunga kwa dili la Pauni 24 milioni, lakini kabla hajaondoka Bayern, alizungumza vitu vilivyomfanya Gravenberch ashawishike kwenda kukipiga Anfield.

“Sadio ni mtu mzuri, kijana mzuri sana,” alisema Gravenbarch na kuongeza: “Nilipokuwa Munich, nilimuuliza kuhusu Liverpool. Kama ilikuwa hatua muhimu kwangu kwenda, jinsi gani klabu ilivyo. Alisema mambo mengi sana mazuri yaliyoniingia kichwani na kusema, ‘lazima niende, lazima niende!’”

Kingine kilichomvutia Gravenberch ni kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, ambaye alimshawishi kwamba akienda Anfield atakwenda kupata nafasi ya kucheza, lakini anachopaswa kufanya ni kuhakikisha anatoa huduma bora anapokuwa uwanjani.