Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benin yachimba mkwara mzito

BENIN Pict

Muktasari:

  • Benin ilicheza mashindano yao ya kwanza ya Afcon mwaka 2004, lakini miaka ya karibuni timu hiyo imekabiliwa na changamoto nyingi na timu hiyo ilishindwa kufuzu mashindano ya Afcon 2021 na 2023.

CASABLANCA, MOROCCO: BENIN imepanga kufanya vizuri kwenye mashindano ya Afcon 2025 ikiamini imeandaa kikosi chake kwa ajili ya kuonyesha makali ya hali ya juu wakati kikishiriki kwa mara ya tano mikikimikiki hiyo ya ubingwa wa Afrika.

Benin ilicheza mashindano yao ya kwanza ya Afcon mwaka 2004, lakini miaka ya karibuni timu hiyo imekabiliwa na changamoto nyingi na timu hiyo ilishindwa kufuzu mashindano ya Afcon 2021 na 2023.

Baada ya kukaribia kabisa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, kocha msaidizi na mkuu wa idara ya kusaka vipaji, Tunde Adelakun anaamini watahamishia makali yao kwenye mashindano ya Afcon 2025, kama walivyofanya kwenye Afcon 2019 na timu hiyo ilifika hatua ya robo fainali.

BEN 02

"Nataka timu yangu ichezea soka maridadi," amesema Adelakun.

"Ningependa kushinda mashindano haya. Safari yetu itakuwa ngumu, lakini tumejifunza kwa mengi kutokana na mashindano yaliyopita ya Afcon."

Kocha mkuu wa Benin, Gernot Rohr ametaja kikosi chenye wachezaji waliofanya vizuri kwenye mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, akiwamo nahodha wa kikosi, Steve Mounie.

BEN 01

Kwenye michuano hiyo ya Afcon 2025 inayoendelea huko Morocco, Benin imepangwa kwenye Kundi D sambamba na timu za Senegal, DR Congo na Botswana.

"Kushindwa kufuzu Kombe la Dunia ni maumivu makali tuliyoyapitia," amesema Adelakun na kuongeza.

"Hilo tumeachana nayo, hatujutii tena na tunajivunia kwa kile tulichokifanya. Ni wakati wa kwenda kwenye mashindano ya Afrika na kuhakikisha tunaonyesha dunia kile tunachoweza kukifanya."

Benin itarusha kete ya kwanza kwenye Afcon 2025 kwa kumenyana na DR Congo, Jumanne, timu ambayo ilizichapa Cameroon na Nigeria kwenye mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026.