Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosnia yajipigia Qatar, ikisubiri hatma yake

Muktasari:

  • Timu hiyo ilitumia dakika 29 kupata bao lake la kwanza, likifungwa na Kerim Alajbegovic kwa shuti kali, akitangulia kuwapangua mabeki wa Qatar, akipokea asisti ya Ivan Basic.

Bosnia and Herzegovina imefanikiwa kuibuka na ushindi mzuri wa mabao 3-1 dhidi ya Qatar ikimaliza mechi za makundi huku ikisubiri hatma yake ya kufuzu mtoano.

Timu hiyo ilitumia dakika 29 kupata bao lake la kwanza, likifungwa na Kerim Alajbegovic kwa shuti kali, akitangulia kuwapangua mabeki wa Qatar, akipokea asisti ya Ivan Basic.

Bosnia ikapata bao la pili  dakika ya 34 baada ya kipa  wa Qatar Mahmoud Abunada kujifunga wakati akipambana kuokoa shuti la mshambuliaji Edin Dzeko.

Qatar ikafanikiwa kurudi mchezoni baada ya kupata bao dakika ya 42 likifungwa na kiungo Hassan Al Haydos akipokea krosi ya Edmilson Junior, timu hizo zikienda mapumziko huku Bosnia ikiongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili timu hizo zikiendelea kushambuliana kwa zamu lakini ilikuwa Bosnia iliyofanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 80 mfungaji akiwa kiungo Ermin Mahmic akimalizia shambulizi la piga nikupige kwenye lango la Qatar.

Mpaka mwisho wa mchezo Bosnia ikafanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-1, ikijihakikishia nafasi ya tatu, baada ya kukusanya pointi nne katika kundi B, ikilingana na Canada iliyopo nafasi ya pili lakini zikitofautiana kwa mabao ya kufungwa na kufunga.

Switzerland ndio vinara wa kundi hilo B ikimaliza na pointi saba wakati Qatar ikiishia hatua ya makundi baada ya kuambulia pointi moja pekee.

Bosnia sasa inasubiri hatma yake ya kwenda hatua ya 32 bora kupitia mlango wa 'best looser' ikisubiri matokeo ya timu zingine zitakazomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi yao.

Timu nane zitakazomaliza nafasi ya tatu na kuwa na matokeo mazuri kwa makundi yote 12, zitafuzu hatua ya 32 bora zikiungana na zitakazomaliza nafasi mbili za juu kukamilisha idadi ya mtoano.