KOMBE LA DUNIA QATAR 2022: Mziki mnene humu ndani

DOHA, QATAR. KUMEKUCHA. Timu 32 zitaonyeshana ubabe kwenye mechi 64, zitakazopigwa kwenye viwanja vinane. Bingwa mmoja tu.
Ni mwendo wa fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazopigwa huko Qatar, ambapo mziki wake utaanza rasmi Novemba 20 kwenye mechi ya ufunguzi na fainali yake itakuwa Desemba 18. Mchakamchaka wote huo utafanyika kwenye viwanja vya kibabe kabisa.
Viwanja mahususi kwa fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar ni Lusail Iconic uliopo Lusail, Al Bayt Stadium uliopo Al Khor, Al Janoub Stadium uliopo Al Wakrah, Ahmad Bin Ali Stadium, Khalifa International Stadium na Education City Stadium vilivyopo kwenye mji wa Al Rayyan na Stadium 974 na Al Thumama Stadium vinavyopatikana Doha. Viwanja vyote hivyo vimejengwa ndani ya eneo la kilomita 55 kuzunguka mji mkuu wa Qatar, Doha. Mwali wa Kombe la Dunia 2022 atasakwa humu.
LUSAIL STADIUM
Uwanja wa Taifa wa Lusail utatumika kwenye mechi 10 za Kombe la Dunia 2022, zikiwamo sita za makundi na nyingine za mtoano ikiwamo ya fainali. Mwonekano wa uwanja huo ni kama bakuli.
Uwezo: Watazamaji 80,000
Uzinduzi: 2022
Mechi zitakazopigwa
Novemba 22; Kundi C: Argentina v Saudi Arabia
Novemba 24; Kundi G: Brazil v Serbia
Novemba 26; Kundi C: Argentina v Mexico
Novemba 28; Kundi H: Ureno v Uruguay
Novemba 30; Kundi C: Saudi Arabia v Mexico
Desemba 2; Kundi G: Cameroon v Brazil
Desemba 5; 16 bora: 1H v 2G
Desemba 9; Robo fainali: W49 v W50
Desemba 13; Nusu fainali: W57 v W58
Desemba 18: Fainali
KHALIFA INTERNATIONAL
STADIUM
Uwanja wa Khalifa International utatumika kwenye mechi nane za Kombe la Dunia 2022, ikiwamo sita za hatua ya makundi, mechi moja ya hatua ya mtoano ya 16 bora na kipute kingine kitakachopigwa hapo ni cha kusaka mshindi wa tatu.
Uwezo: Watazamaji 40,000
Uzinduzi: 1976
Mechi zitakazopigwa
Novemba 21; Kundi B: England v Iran
Novemba 23; Kundi E: Ujerumani v Japan
Novemba 25; Kundi A: Uholanzi v Ecuador
Novemba 27; Kundi F: Croatia v Canada
Novemba 29; Kundi A: Ecuador v Senegal
Desemba 1; Kundi E: Japan v Hispania
Desemba 3; 16 bora: 1A v 2B
Desemba 17; Mshindi wa tatu.
STADIUM 974
Stadium 974 utatumika kwenye mechi saba za fainali za Kombe la Dunia 2022, sita za hatua ya makundi na moja ya mtoano kwenye hatua ya 16 bora. Uwanja huo umejengwa kwa makontena na vyuma ukiwa na mwenekano wa kipekee kabisa kwa mashabiki.
Uwezo: Watazamaji 40,000
Uzinduzi: 2021
Mechi zitakazopigwa
Novemba 22; Kundi C: Mexico v Poland
Novemba 24; Kundi H: Ureno v Ghana
Novemba 26; Kundi D: Ufaransa v Denmark
Novemba 28; Kundi G: Brazil v Uswisi
Novemba 30; Kundi H: Poland v Argentina
Desemba 1; Kundi G: Serbia v Uswisi
Desemba 5; 16 bora: 1G v 2H
AL BAYT STADIUM
Uwanja wa Al Bayt utatumika kwenye mechi tisa za Kombe la Dunia 2022, ikianzia ya ufunguzi na nyingine tano za hatua ya makundi na mechi tatu za hatua ya mtoano. Mwonekano wake ni kama mahema ukiwakilisha historia watu wa kuhamahama.
Uwezo: Watazamaji 60,000
Uzinduzi: 2021
Mechi zitakazopigwa
Novemba 20; Kundi A: Qatar v Ecuador
Novemba 23; Kundi F: Morocco v Senegal
Novemba 25; Kundi B: England v Marekani
Novemba 27; Kundi E: Hispania v Ujerumani
Novemba 29; Kundi A: Uholanzi v Qatar
Desemba 1; Kundi E: Costa Rica v Ujerumani
Desemba 4; 16 bora: 1B v 2A
Desemba 10; Robo fainali: W51 v W52
Desemba 14; Nusu fainali: W59 v W60
AHMAD BIN ALI STADIUM
Uwanja wa Ahmad bin Ali utatumika kwenye mechi saba za Kombe la Dunia 2022, sita za hatua ya makundi na moja kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora. Uwanja huo umejengwa kwa dizaini za kibabe kabisa kuwakilisha utaduni na uzuri wa jangwani.
Uwezo: Watazamaji 40,000
Uzinduzi: 2020
Mechi zitakazopigwa
Novemba 21; Kundi B: Marekani v Wales
Novemba 23; Kundi F: Ubelgiji v Canada
Novemba 25; Kundi B: Wales v Iran
Novemba 27; Kundi B: Japan v Costa Rica
Novemba 29; Kundi B: Wales v England
Desemba 1; Kundi F: Croatia v Ubelgiji
Desemba 3; 16 bora: 1C v 2D
AL THUMAMA STADIUM
Uwanja wa Al Thumama utatumika kwenye mechi nane za fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, ambapo mechi sita ni za hatua ya makundi na mbili zitakuwa za hatua ya mtoano. Dizaini inawakilisha baraghashia, kofia za kufuma kwa uzi za wanaume.
Uwezo: Watazamaji 40,000
Uzinduzi: 2021
Mechi zitakazopigwa
Novemba 21; Kundi A: Senegal v Uholanzi
Novemba 23; Kundi E: Hispania v Costa Rica
Novemba 25; Kundi A: Qatar v Senegal
Novemba 27; Kundi F: Ubelgiji v Morocco
Novemba 29; Kundi B: Iran v Marekani
Desemba 1; Kundi F: Canada v Morocco
Desemba 4; 16 bora: 1D v 2C
Desemba 10; Robo fainali: W55 v W57
AL JANOUB STADIUM
Uwanja wa Al Janoub utatumika kwenye mechi saba za fainali za Kombe la Dunia 2022, ambapo sita zitakuwa za hatua ya makundi na moja kwenye mtoano wa hatua ya 16 bora. Dizaini ya uwanja huo ni kuonyesha utamaduni wa majahazi.
Uwezo: Watazamaji 40,000
Uzinduzi: 2019
Mechi zitakazopigwa
Novemba 22; Kundi D: Ufaransa v Australia
Novemba 24; Kundi G: Uswisi v Cameroon
Novemba 26; Kundi F: Tunisia v Australia
Novemba 28; Kundi G: Cameroon v Serbia
Novemba 30; Kundi D: Australia v Denmark
Desemba 1; Kundi H: Ghana v Uruguay
Desemba 5; 16 bora: 1E v 2F
EDUCATION CITY
STADIUM
Uwanja wa Education City wenyewe utatumika kwenye mechi nane za fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, ambapo sita zitakuwa za hatua ya makundi na mbili ni za mtoano. Umedizainiwa kuwakilisha almasi zinazopatikana Mashariki ya Kati.
Uwezo: Watazamaji 40,000
Uzinduzi: 2020
Mechi zitakazopigwa
Novemba 22; Kundi D: Denmark v Tunisia
Novemba 24; Kundi H: Uruguay v Korea Kusini
Novemba 26; Kundi C: Poland v Saudi Arabia
Novemba 28; Kundi H: Korea Kusini v Ghana
Novemba 30; Kundi D: Tunisia v Ufaransa
Desemba 2; Kundi H: Korea Kusini v Ureno
Desemba 6; 16 bora: 1F v 2E
Des 9; Robo fainali: W53 v W54.