Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola hashtuki KDB kusakwa Anfield

Muktasari:

  • Kocha Guardiola alisema anachofanya ni kumwombea tu heri kiungo huyo pamoja na familia yake na hajali timu gani atakwenda kujiunga nayo hata kama ni wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa kwenye Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya kuibuka kwa uvumi Liverpool inafanya mchakato wa kunasa huduma ya Kevin De Bruyne limemuibua kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.

Kocha Guardiola alisema anachofanya ni kumwombea tu heri kiungo huyo pamoja na familia yake na hajali timu gani atakwenda kujiunga nayo hata kama ni wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa kwenye Ligi Kuu England.

De Bruyne amekuwa staa muhimu kwenye mafanikio ya Man City kwa kipindi cha muongo mmoja, akicheza mechi 400, akifunga mabao 108 na asisti 177.

Mataji mawili kati ya sita aliyobeba Ligi Kuu England alichuana jino kwa jino na Liverpool. Sasa akielekea umri wa miaka 34, De Bruyne alitangaza ataachana na maisha ya Etihad msimu huu utakapofika tamati.

Liverpool bado haijapeleka ofa rasmi ya kumtaka kiungo huyo, lakini mipango yao ni kunasa huduma ya kiungo ambaye atakuja kuongeza kitu cha ziada kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mdachi, Arne Slot.

Uzuri ni kwamba De Bruyne mwenyewe hajafuta uwezekano wa kujiunga na moja ya timu wapinzani wa Man City kwenye Ligi Kuu England ili kubaki katika ligi hiyo yenye ushindani mkali.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa De Bruyne kwenda kujiunga na timu pinzani, Guardiola alisema: “Sifahamu, namtakia kila la heri Kevin kwake na familia yake.”.

De Bruyne amekuwa akihusishwa na Liverpool kwa kipindi kirefu kwenye maisha yake ya soka, tangu kipindi akiwa na umri wa miaka 11, alipokuwa kwenye kikosi cha vijana cha Genk wakati alipofichua kwamba alikuwa akiishabiki timu hiyo ya Anfield mwanzoni mwa miaka ya 2000. Aston Villa nayo inaripotiwa inamfuatilia De Bruyne, wakiamini uzoefu wake utawapa nguvu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku sehemu nyingine anayoweza kwenda Mbelgiji huyo ni Napoli ya Italia.

Kocha Slot alisema: “Kama hakuna namna yoyote ya sisi kuboresha kikosi chetu, basi tutakuwa na tatizo kwa sababu ninachokifahamu kwa asilimia zote, Man City na Arsenal zitaboresha vikosi vyao.”